Tujikumbushe japo kidogo mazuri na mabaya yake:
Safari ya Ole Gunnar Solskjaer ndani ya manchester united
Yawezekana utawala wa Ole Gunnar Solskjaer akiwa kama ni kocha wa muda pale mitaa ya carrington (interim manager)umeshasahaulika baada ya miaka mitatu kupita tokea ateuliwe kuwa kocha mkuu wa manchester united, lakini sidhani kama kuna mshabiki wa manchester united atasahau tukio la comeback lililofanywa na man utd dhidi ya PSG kwenye hatua ya mtoano ya michuano ya champions league huku Ole akiwa bado ni kocha wa muda (man utd walipata ushindi wa magoli 3 dhidi ya 1). Hapo ndipo ulipozaliwa ule wimbo wa "Ole at the wheel"
Baada ya takribani miaka mitatu kupita hatimaye utawala wake umemalizika kwa kufukuzwa kazi baada ya kuendelea kupata matokeo yasioridhisha huku yale yote alioyazungumza kupitia mahojiano yake ya mwanzo juu ya style ya kiuchezaji akishindwa kuyasimamia ipasavyo kwa mtazamo wangu Mimi.
furaha na dhoruba kwa wakati mmoja
Baada ya kumalizika kwa mechi dhidi ya PSG, Ole gunnar alihudumu mechi mbili tu akiwa na nyadhifa ya ukocha wa muda (caretaker) wa manchester united na mechi hizo ziliishia kwa man utd kuambulia vipigo ikiwemo mechi ya Barcelona na baada ya hapo bodi ikaendekea kumuamini na hatimaye akateuliwa kuwa kocha mkuu wa manchester united.
kiuhalisia ulimwengu wa bwana Ole kwa upande wa mfumo rasmi wa kiuchezaji, fikra, na mipango aliyokuja nayo tokea mechi ya kwanza (tactical perspective) uliishia usiku ule tuliofungwa magoli 2 dhidi ya PSG ndani ya Old trafford na baada ya hapo kila kitu kikabadilika (wengine wakasema honeymoon imeisha) kwa sababu tofauti ikiwemo majeruhi ya wachezaji muhimu.
Ole alirithi timu iliokosa umoja ndani na nje ya uwanja, licha ya kuwepo kwa mazingira mabaya ndani ya kikosi Ole pia alirithi timu iliokwisha poteza pattern ya kiuchezaji na identity. Ole pia alirithi timu iliokwisha onyesha madhaifu makubwa sana kwenye safu ya ulinzi baada ya kuruhusu magoli 29 kwenye mechi 17.
Jose anafukuzwa, Ole anaanza kazi rasmi:
mechi ya kwanza chini ya utawala wa Ole tulianza na mfumo wa 4-3-3 na high pressing system , mechi ya kwanza tulianza na midfield ya matic, herrera na pogba huku safu ya ushambuliaji tulianza na martial, rashford na lingard.
Kwa aliyesikiliza mahojiano ya ole atakuwa anayakumbuka maneno matamu aliyoyaongea, alisema anataka kuona wachezaji wake wanakimbia sana, pressing ya hali ya juu (chini ya ole, pressing intensity ilikuwa ni 8 ukilinganisha na 10 ya jose mourinho, kwa ufupi tuliimarika zaidi na zaidi chini ya ole ukilinganisha na jose chini ya miaka yake miwili), pasi za haraka za kwenda mbele ndio maana si ajabu alianza na watu watatu hao safu ya mbele na hapo katikati akifaidika na uwepo wa pumzi ya ander herrera aliye kwenye ubora, pogba akitokea upande wa kushoto kama alivyokuwa juventus.
Jesse lingard alikuwa ndiye mzungukaji mkuu wa ndani ya uwanja akiongeza work rate hapo juu na chini, kwa ufupi jesse alisimama kama ni kiunganishi kikuu cha safu ya kiungo na ushambuliaji. Uwepo wa jesse, herrera na matic kiulinzi kulimzawadia uhuru wa kiuchezaji paul pogba kwa mara ya kwanza.
Uhuru huo aliutumia vizuri sana paul pogba kwani alifunga magoli matano (non penalty) ndani mechi 9 za mwanzo za ole gunnar, pia aliweza kuongeza assist nne ndani ya hizo mechi 9, kiwango cha kupiga mashuti kiliongezeka kutoka 2.93 chini ya mourinho hadi 4.08
marcus rashford naye kiwango chake cha kupiga mashuti kiliongezeka kutoka 2.0 chini ya mourinho kwa dakika 90 hadi 4.8 huku pia akifunga magoli 6 ndani ya hizo mechi 9 za mwanzo za Ole gunnar. pia ndani ya mechi 10 tulishuhudia mabadiliko makubwa sana ya kiuchezaji, kitakwimu na kimatokeo,
- kwa mfano non-penalty xG ( expected goal) per game tulipanda sana kutoka 1.41 chini ya jose hadi 1.90 chini ya Ole.
- non-penalty xG against tulishuka kutoka 1.43 chini ya jose kwenda 1.07(safu yetu ya ulinzi iliimarika, hatukuwa tunakaribisha mashambulizi ya mara kwa mara)
================
Inaendelea