Ole na mkataba wa kudumu
licha ya kuanza kupata matokeo yasioridhisha ndani ya muda mfupi hilo halikuwazuia watendaji wakuu wa man utd kutokumpa kandarasi ya miaka mitatu ole gunnar solskjaer, wapo baadhi ya wadau waliamini bado haukuwa muda muafaka kumhukumu ole gunnar solskajer (nyakati zile hawa walionekana na wachukiaji) na baadhi yetu tulio wengi tuliamini Ole ndiye mwanadamu pekee mwenye uwezo wa kuitandaza tena DNA ya klabu iliokuwa inapotea kwa kasi ya ajabu hivyo alistahili mkataba wa kudumu licha ya kwamba bado tupo katikati ya msimu.
majeruhi ya wachezaji muhimu na athari zake
yawezekana zipo sababu nyingi sana zilizopelekea Ole aanze kuonja joto ya jiwe pale klabuni lakini hatuwezi kuiondoa sababu ya majeruhi ya wachezaji wetu muhimu kuwa ni kikwazo kimojawapo kilichopelekea dunia imuangalie Ole kwa jicho jengine, wengine walihitaji kumuona Ole anadhihirisha ubora wake kwa malighafi alizonazo.
dakika 90 za mechi dhidi ya PSG ziliharibu kwa kiasi kikubwa ile imani ilioanza kujengwa na mashabiki mbali mbali wa mchezo wa soka dhidi ya ole, kwa kuanzia majeruhi ya lingard na martial ndani ya dakika 45 za kipindi cha kwanza, licha ya kwamba wachezaji wote hao wawili hawakuwa na takwimu nzuri za kiufungaji lakini uwepo wao uwanjani ulikuwa ni faida tosha ya kimfumo.
Miguu iliochoka ya alex sanchez na juan mata ndio ililazimika kutumiwa na Ole gunnar solskjaer kuziba nafasi ya majeruhi, both sanchez na mata hawakuwa na uwezo wa kuendana na falsafa mpya za mwalimu kutokana na kukosa kwao fitness pamoja na kasi ya kukimbia.
siku chache baadae man utd wakiwa wanajiandaa na mechi dhidi ya liverpool zikazuka taarifa rasmi za kupata majeruhi kwa nemanja matic.
Ilipofika mechi ya liverpool tulishuhudia ndani ya dakika chache tokea kuanza kwa mechi mchezaji mwengine muhimu kwenye ule mfumo wa 4-3-3 akipata majeruhi na hapa namzungumzia ander herrera na nafasi yake ilizibwa na andreas perreira.
kimiujiza mchana huo tulishuhudia kurudi uwanjani kwa jesse lingard na kutokana na ufinyu wa kikosi ole alilazimika kumtumia jesse lingard licha ya kwamba bado hakuwa fiti kimapambano, mchana huo tulishuhudia kwa mara nyengine tena jesse lingard akipata majeruhi na nafasi yake kuzibwa na juan mata.
mchana huo huo pia tulishuhudia tukio jengine la kusikitisha lililomhusu mchezaji mwengine muhimu anayeunda mfumo ule wa 4-3-3, hapa namzungmzia marcus rashford na jinamizi la majeruhi alilolipata baada ya kuchezewa rafu na jordan henderson.
Licha ya rashford kuendelea kucheza ndani ya mechi hiyo ila hakuwa tena na uwezo hata wa kukimbia jambo lililopelekea unite waonekane kuwa na wachezaji 10 kwa 11, baada ya hapo marcus rashford naye alianza rasmi jinamizi hilo la majeruhi.
mabadiliko ya tactics
majeruhi ya wachezaji takribani wanne muhimu ndani ya kikosi cha kwanza yalimfanya Ole afikirie njia mpya ya kutengeneza kikosi chake kwa kutumia mfumo mwengine wa kiuchezaji kutokana na kundi la wachezaji waliopo na hapo ndipo tulipoanza kuufahamu upande wa pili wa Ole, si hivyo tu hapo ndipo Ole na makocha wengineo mfano wake wanaokutana na changamoto ya majeruhi wanapopaswa kutuonyesha upande wa pili wa ufundi wao (kupata matokeo bora kwa malighafi ulizonazo).
Majeruhi yalipelekea tushuhudie mabadiliko ya mara kwa mara ya mifumo ya kiuchezaji, zipo baadhi ya mechi tulicheza na 4-4-2 diamond tukimtegemea juan mata, zipo baadhi ya mechi tulicheza 4-3-3 tukimtegemea sanchez eneo la ushambuliaji huku romelu lukaku akicheza winga licha ya kwamba kiasili yeye ni namba 9 mahiri kuliko wengineo tuliokuwa nao kipindi hicho.
kwa ufupi baada ya kuvurugika kwa ile 4-3-3 aliyoanza nayo siku ya kwanza ya kukabidhiwa timu bwana OIe hakuwa na mfumo rasmi wa kiuchezaji na kubaki na ubabaishaji (labda tuseme hakuwa anawafahamu wachezaji wake).
majeruhi ya matic na herrera yalizalisha tatizo la ukosefu wa ball progressing, ball winners kwa wachezaji waliorithi nafasi zao (namzungumzia fred, mctominay, perreira) jambo lililokuwa linamlazimu paul pogba afanye majukumu ya kutafuta mpira chini na kucheza long pass kwa safu ya ushambuliaji.
kurudi kwa wachezaji walio majeruhi
licha ya kwamba baadhi ya wachezaji muhimu waliweza kurudi uwanjani lakini bado hali yakiuchezaji ilishindwa kuimarika kwa kiwango kilichozoeleka na hapo ndipo ubora wa ole juu ya game managements ulipozidi kujadiliwa
- rashford alifunga goli 1 badala ya lile alilofunga dhidi ya psg (naruhusu marekebisho)
- romelu lukaku (winga teleza wa Ole) alishindwa kufunga goli, martial naye alifunga goli 1
- manchester united walicheza dakika 530 bila ya kufunga kupitia open play.
kunyimwa mkataba kwa ander herrera
chini ya ole tulishuhudia kupewa mkataba mpya kwa scott mctominay ambaye alionekana kama ni damu mpya ndani ya kikosi cha man utd tokea alipoanza kupewa nafasi na ole dhidi ya liverpool pia tulishuhudia kutokufikiwa kwa makubaliano ya kimkataba dhidi ya herrera na hatimaye jamaa akatangaza kuondoka kikosini dirisha lijalo.
tukumbuke katikati ya ligi baada ya kupata majeruhi kwa ander herrera wachezaji waliopo walishindwa kuziba nafasi yake kiufasaha na naamini mpaka leo hii bado tumeshindwa kupata ile chemistry ya kiuchezaji tulioishuhudia kutoka kwake tunapoanza na fred mctominay.
kupewa mkataba mpya kwa martial
baada ya kuteuliwa kuwa kocha mkuu, ole alihitaji kujenga timu itakayoongozwa na fikra zake mwenyewe na alianzia kwanza safu ya ushambuliaji kwa kumpa kandarasi mpya martial aliyeamini ndiye namba 9 sahihi kwenye kikosi kwa msimu ujao (lukaku alianza kucheza kati mechi za mwisho licha ya baadhi ya wachezaji kurudi)
Martial huyu aliyepewa kandarasi mpya ya miaka 5 cha kustaajabisha alifunga magoli mawili ndani ya muda wote wa uongozi wa Ole kama nitakuwa sahihi.
- Je martial alistahili kuwa mshambuliaji badala ya lukaku?
- je herrera ulikuwa ni muda muafaka kwake kuondoka kwa kuwategemea scott, perreira na fred?
======================