Bavaria
JF-Expert Member
- Jun 14, 2011
- 53,092
- 53,568
Waingereza ni wachezaji wanaofanya vizuri msimu mmoja, unaofuatia wanakata moto.We are an awfully coached team, jamaa sijui aliwaza nini mwaka mmoja uliopita mpaka akaanzisha thread hii kwenye forum ya redcafe
- Dakika 10 za Donny van de beek zimeleta matumaini kuliko dakika nyingi za Paul pogba, Donny anaonewa bila ya sababu.
- Back 3 bila ya proper wingback ni kujihashua,Shaw na wan bissaka bado hawatoshi.
- Luke shaw amekata moto, huenda zile sifa za kijinga alizokuwa akipewa na waingereza wenzake kwenye michuano ya kombe la euro zilimjaza upepo wa kijinga, eti walikuwa wanamwita shawberto Carlos.
- Bila ya winga hatuna makali, si ajabu kipindi cha kwanza tulidhibitiwa vilivyo kwa sababu hatuna uwezo wa kupita katikati, nilifurahi alipoumia mlinzi mmoja(natumai atarudi mapema uwanjani)na kuswitch mfumo.
- Wan bissaka ameimprove anapokuwa na mpira lakini bado hatoshi kuwa mchezaji wa Manchester united.
- hivi harry Maguire anamzidi mlinzi yupi kati ya wale watatu tulionao, ni lini benchi la ufundi watakisikia kilio cha mashabiki waliowengi duniani wanaokerwa na performance mbovu ya Maguire kila wiki, harry Maguire na Phil Jones ni ndugu wawili wasiojuana kifamilia. Kwani kuna ubaya kwa mwanadamu kukiri makosa yake alioyatenda, mbona ole amekuwa mgumu kumpumzisha huyu jamaa (hata msema ovyo paul scholes ameonyesha kukerwa na kiwango chake duni).Leicester wametubikiri hadharani.
- Scott mctominay ni press resistance asiyejitambua, uoga na upumbavu wa maamuzi umemjaa miguuni na kichwani, huenda hana bando la kumuwezesha kuangalia video za Marco verratti, bosquet,kovacic,moussa dembele n.k
- Tulishawahi kuifikiria partnership ya Eric Bailly na Raphael varane japo kwa mchana mmoja?.......NEPOTISM ni ugonjwa mbaya sana.
- CR7 ni mbuzi wa miongo miwili(g.o.a.t), anatufurahisha na muda huo huo anatukera.
- Nimeikumbuka ile thread yenye kichwa cha habari kifuatacho
Ukisikia kusafiri kwa muda ndio mfano wa thread hiyo, wengi tumeanza kumuelewa.
We are an awfully coached team
Yes, we are. No plan, no pattern or no style. Just a bunch of 11 individuals on the ground trying to do something. Bringing a right back who can attack because our 50m signing cant attack. Playing Bruno deep , Rashford right, Cavani left. Seriously WTF is happening?www.redcafe.net
Hapo united, nioneshe muingereza anaefika levels za Bruno? Halafu angalia bei zao.
Ukienda nchi zingine unapata wachezaji quality kwa bei nafuu. Ila tupo busy kununua waingereza kwa bei kubwa.
Maguire akacheze Aston Villa, Bissaka aende Crystal Palace, Shaw aende Arsenal huko, McTomminay aende hata Blackburn. Hawa ni wa kucheza vitimu vya ajabu. Sio wavae badge ya timu kama Man Utd.