Forgotten
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 3,630
- 11,096
4-2-3-1 ni mfumo mzuri unaoifanya timu kuwa vizuri katika maeneo mawili kwa pamoja: defensively na offensively. Kinachofelisha huu mfumo ni mapungufu ya watu sahihi kwenye namba ya kiungo mkabaji.Tulimwambia akitaka matokeo aachane na 4 2 3 1.
3-5-2 ni mfumo mzuri ila ni mfumo ambao kwa timu yetu unaweza usifanye kazi ipasavyo tukikutana na timu imara. Mfumo huu utatufanya tuwe defensively wazuri ila kucheza na playmaker mmoja huku tukiwategemea Shaw na AWB ni kama tutakosa vitu baadhi kwenye huu mfumo. Mfumo unahitaji zaidi LWB na RWB wanaopandisha mashambulizi na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga kwa washambuliaji. Telles na Dalot ni option nzuri zaidi katika mfumo huu.
Kama Ole anataka ku-stick na huu mfumo kwa kuwatumia Shaw na AWB ni heri Pogba akirudi a-switch kwenda 3-1-4-2 ila itabidi McFred ivunjwe sasa sijui nani atafaa kusimama katika DM. 3-1-4-2 itatufanya tuwe hatari zaidi kwa kutumia playmaker wawili Pogba na Bruno maana kule mbele Ronaldo na Cavani wao wanasubiri kutengenezewa tu nafasi za kufunga.
January wafanye wapate DM tu-switch kwenye 4-3-3 naamini hii timu iliundwa kuja kutumia huu mfumo in the future. Next summer I hope tutapata a long-term striker (Haaland).





#MUFC



