Manchester United (Red Devils) | Special Thread

yes jamaa alisumbua sana alivyoingia pia nimegundua chelsea wanabeki ngumu sana asee kupita ufanye kazi hasa.
Ruben Loftus Cheek alicheza dakika chache sana dhidi ya city ila alionesha kitu ambacho timu yetu viungo walishindwa kufanya kwa dakika 90
 
Gary Neville on Manchester United:
“I think you have to be a unit in and out of possession, and when you only deliver in moments, those moments won’t go for you in certain games. You need patterns of play, way of playing — I still see a group of individuals playing in moments.”
================

huyu kocha mbovu wa zamani wa valencia anapata wapi jeuri hii ya kumnanga baby face kutoka norway, alikuwa wapi kwa kipindi chote hicho mpaka ajitokeze leo hii kuzungumzia ishu ya structure, pattern of plays haliyakuwa sisi tuliokuwa huku uswahili na tusio na taaluma yeyote ya kimpira tumekuwa tukilizungumzia swala hili kwa miaka mitatu. si ndiye gary neville huyu aliyeuliza eneo gani lijengwe sanamu la ole baada ya kuwatoa PSG kwa kikosi dhaifu
=================

ujio wa thomas tuchel ndani ya chelsea umekuwa ni faida kwa upande wa chelsea kwa sababu ya mafanikio alioyaleta kwa kubeba makombe, pia kitendo cha thomas tuchel kuimpelement falsafa ngeni ya kiuchezaji ndani ya chelsea na kueleweka kwa muda mfupi na wachezaji pia linaweza kuwa ni tusi kubwa kwa kocha wetu ambaye mpaka mchana wa leo hajulikani anachokisimamia ndio maana si ajabu hata rafiki yake anayeitwa gary ameonekanwa kushitushwa mwenendo wa timu kiuchezaji na si kimatokeo. Ole ana takwimu bora sana kuliko kocha mwengine wowote baada ya kuondoka kwa ferguson kimatokeo na rekodi nyenginezo ukiondoa makombe ndio maana mjadala wake unakuwa ni mgumu..

mimi bado nina imani na ubora wa kikosi kilichopo tunaweza kufanya vizuri, sikubaliani na mawazo ya wengineo wanaojaribu kuonyesha matatizo fulani kuwa ndio sababu ya timu kufanya vibaya kiuchezaji na baadae kimatokeo, kumekuwepo na vuguvugu la kuwalaumu wachezaji wanaocheza CDM (fred, matic, scott) na RB (wan bissaka, dalot) kuwa ni kikwazo cha timu kucheza vizuri. Kocha bora mfano wa klopp ameweza kumfanya jordan henderson aonekane kuwa ni mchezaji bora mbele ya hadhira japokuwa wengi wetu hatuamini hivyo yote ni kwa sababu amemtengenezea structure ilio bora.

ndani ya muda mfupi tumeshuhudia thomas tuchel akiwasuka baadhi ya wachezaji na kuwafanya waonekane tishio haliyakuwa mwanzoni walionekana ni wa kawaida na waliokwishapitwa na wakati, baadhi ya wachezaji hao ni jorginho, rudiger, thiago silva, christensen.

Legendary Fergie aliweza kuwafanya zaidi wachezaji 20 wenye viwango vya wastani kuonekana kuwa ni wa umuhimu ndani ya kikosi na hatimaye waliweza kuwa sehemu ya vikosi tofauti vilivyoshinda makombe makubwa kwa mihula tofauti (fletcher, sylvestre, oshea, phil neville, wes brown, quinton fortune). Kwa mukhtadha huo ni wajibu wa kocha kutransform kiwango cha mchezaji husika kutoka level moja kwenda nyengine na si tu kusubiria kila tatizo litatuliwe kwa njia ya usajili.

Ni kipofu pekee ndiye atakayepingana na huu ukweli wa kwamba tatizo letu kubwa lipo kiufundishwaji zaidi na si wachezaji tunaopenda kuwatoa kafara ( lack of a well-drilled structure and pattern of play). ukitaka kuuona kwa uwazi kabisa udhaifu wa mwalimu wetu eneo la structure ya kiuchezaji jaribu kumchunguza siku anayofanya rotation ya wachezaji, wakati zipo timu mfano man city, liverpool hata kama watabadili nusu ya kikosi bado pattern ya kiuchezaji inabaki kuwa ni ile ile.

pia kutokuwa na mchezaji bora kwenye eneo moja au mawili haiwezi kuwa sababu ya timu kucheza na presha kubwa kila wiki, Ole anahitaji kufanya mapinduzi makubwa ya kimbinu kwa takribani mechi zote na si kusubiria mechi kubwa (hapa anakuwa anajiandaa vizuri sana mpaka tunashangazwa).

kama yeye ameshindwa basi asione tabu kufanya mapinduzi ya benchi lake la ufundi either kwa kuajiri assitant mwenye uzoefu au hata kwa kumtafuta rafiki yake aliyepo molde anayeitwa eric laurie anayejishughulisha na ukufunzi pamoja na uchambuzi wa mifumo ya kiuchezaji (sipo serious), teh teh bila ya shaka fuentte anamfahamu. Kama ameweza kuleta kocha maalumu wa kufundisha set piece basi na hayo maeneo mengine ayatazame kwa jicho ang'avu

Hata sir alex ferguson kwa nyakati tofauti tulishuhudia akifanya mabadiliko ya benchi la ufundi kwa sababu tofauti, kwa mfano aliwahi kufanya kazi na Brian Kidd (kwa sasa yupo man city kwa takribani miaka 10), Rene Meulensteen, carlos queroz (hapa tukashuhudia mapinduzi ya mifumo kama 4-3-3, steven mcClaren, Walter Smith japo kwa muda mfupi, Archie Knox (huyu alifanya naye kazi akiwa aberdeen na baadae manchester united).

Moyoni sifurahishwi kabisa na kelele za kumuondoa Ole Gunnar kwa sababu ya alichotufanyia akiwa mchezaji na haya mapinduzi yake ya ujengaji wa timu, ametufanya tuhame katika dunia ambayo tulikuwa hatufahamu changamoto kubwa za timu yetu ni zipi mpaka kuikaribia kwa asilimia 80 nchi ya ahadi, leo sote tunafahamu usajili gani tufanye hata dirisha lijalo (RB, DM, CF) na hiyo imetokanwa na kazi bora iliofanywa na Ole kwa kutuanzia upya structure ya ujengwaji wa timu (cha ajabu structure ya kiuchezaji kwa kila wiki ndio inamshinda).

Nitasikitishwa sana kama atakubali kuivunja nyumba hii kwa mikono yake mwenyewe, kwangu mimi nawafikiria zaidi hawa vijana wa academy na mustakabali wao, Je atakuja mwanadamu anayeamini soka la kuwapa nafasi vijana?
======================

mkataba wa kazi haufanani na maagizo ya vitabu vya dini, muda wowote mkataba unavunjika
Hans-Dieter-Flick2.jpg
 
Mkuu bandiko limetulia sana,(nitakushauri kitu baadaye)

Waswahili tuna msemo wetu kuwa ukiwa nje ya ulingo ni rahisi kuona makosa ya mwenzio kuliko ukiwa ndani yake.
Ninaamini kundi lote la legendary wa united (isipokuwa Roy Keane) walishaliona tatizo la united liko wapi isipokuwa tu wote waliogopa kumsema vibaya mshikaji wao Ole. Gary katuonesha kwa mara nyingine tena (baada ya sakata la supa ligi) kuwa anasimama kwa maslahi makubwa ya klabu na wapenzi wa klabu badala ya ushikaji na maslahi ya Ole. Kaonesha njia ninaamini wengine watafuata muda si mrefu.

Nilishawahi kutoa maoni yangu hapa kuwa kwanini tusifanye sajili za kumaliza matatizo karibia kila nafasi uwanjani halafu madirisha yajayo tukawa tunaziba viraka tu kuliko kila msimu tunauanza huku tukijua kwa hakika tunamapungufu makubwa eneo flani? Lakini nikaambiwa hiyo haiwezekani kulingana na bajeti ila Chelsea ya Lampard iliweza na City ya Pep pia ikafanikisha hilo hivyo wenzetu wamekuwa na msingi wa timu imara ila sisi hata Pogba hatuna uhakika naye,Cavan ni kama tumeisha mkosea heshima baada ya ujio wa ronaldo na Ronaldo mwenyewe sio wa kumtegemea misimu miwili ijayo. Na upatikanaji wa Haarland sio kitu rahisi endapo bayern, madrid na psg wakitia makucha yao pale. Kitu nilicho na uhakika nacho baada ya kuiangalia aunited,baada ya kuziba pengo la CDM,tutarudi kukosoa uchezaji wa Wanbisaka na listi itakuwa ikiendelea msimu hadi msimu.

Baada ya kutokea ukosoaji wa namna McFred inavyopunguza nguvu ya kiushambiuliaji,utetezi wa Ole ukawa kwamba hana walinzi imara hivyo hiyo McFred ni kwa ajili ya kuupa ukuta wetu (Maguire na lindelof) uimara. Lakini leo hii kuna Maguire na Varane ila McFred bado iko pale pale haiteteleki. Hii tafsiri yake ni kwamba Ole ni aidha Ole anaogopa kubadili mbinu au anaogopa kuwakwaza baadhi ya wachezaji wnaomfanya aishi mjini pamoja na kuwafurahisha waingereza. Nategemea kuona ni kwa namna gani atalazimisha pogba,bruno,sancho na rashford kukaa kikosi cha kwanza bila kuipangua McFred yake wakati huo huo asiwaudhi waingereza kwa kutomchezesha golden boy Greenwood (Hawa akina VdB,dalot na lindelof anawaweza sababu ya utaifa wao).

Kwa jinsi EPL ilivyo na ushindani hasa katika suala la mbinu,Hans ni mtu sahihi kuja kupambana na Pep,Klopp,Tuchel pamoja na Arteta. Ila Ole anatumia mbinu za mwaka 90 za Fergie dhidi ya hawa wataalam.
 
Licha ya ku-spend karibia £180m+(Maguire,Bissaka,Varane,Telles) kwenye defence lakini still hata kupata clean sheet imekuwa shida
Na bado backline inalindwa na McFred.
Binafsi sioni fahari ya kufanya come back sababu ya uzembe wetu.
 
Watu wanataka DNA ya united wakati ishapitwa na wakati, Ole hio DNA haiwezi na hamna namna mbinu za fergie zinaweza work leo ndo mana mzee alijistaafia zake tuko 21 karne sasa mpira wa janja janja tutasubiri sana kwa watu wa kazi. Ole hatoshi tunampenda sana legendary wetu katupa uefa ila apumzike tu kwakweli.
 
Sir Alex Ferguson has reportedly told Manchester United to sign Peterborough youngster Ronnie Edwards (MF - 18). he could be worth up to £20m in the Future

#theExpress
manutd |
#GGMU
IMG_20210927_200829_800.jpg
 
Back
Top Bottom