Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

"You know Cristiano Ronaldo? One of the greatest players of all time. Yeah, he calls me captain now"
FB_IMG_1630123213183.jpg
 
Umeona impact ya director of football? Jamaa yupo serious, strategic and very fast. Naamini huyu jamaa anaweza kusuka timu imara sana ndani ya hii misimu miwili. Kwa mara ya kwanza tumeingia sokoni tukiwa serious sana toka aondoke David Gill.

Techically, ukiangalia kwa umakini Ed Cavani anamaliza mkataba wake mwakani kama tunawasha moto msimu huu ili u-maintain momentum ya timu unahitaji repalacement makini. Nafasi ya mchezaji kama Cristiano au Lionel ikijileta hulazi damu, ni aina ya mchezaji ambaye hukosi goli 15 za EPL na goli 7 za UEFA kutoka kwao.
Uache kuchukua mtu ambaye kufunga ni kitu cha kawaida uhangaike na wazuia magoli (DM) apo apo unao wengi tu, kwa vyovyote itakavyokuwa tulimhitaji CR7, madrid wangemhitaji CR7, Chelsea wangemhitaji CR7, man city wangemhitaji CR7, Barca wangemhitaji CR7, hakuna timu hapa duniani ingemuacha kama ingepata nafasi hiyo cz impact yake ni kubwa kwa klabu na ligi kwa ujumla.
 
Manchester United shares have soared 9% after the football club announced a sensational deal to re-sign Cristiano Ronaldo. As a result, the club's value increased by about $300m on the New York Stock Exchange. Investors are rubbing their hands
1630128935623.png
 
Mkuu ndio sheria zinasema hivo ,Cavan kashasajiliwa hawezi nyanganywa namba 7 kizembe bila sababu ya msingi ,either aondoke ..

Hakuna namna nyingine ya ronaldo kuvaa jezi no 7.....
Ronaldo atavaa namba 7 na Premier League hawatazuia hilo kwakuwa sheria ina kipengele cha kibali maalumu. CR7 ni brand, United bila shaka watatuma maombi yao na Ronaldo atapata kibali maalumu cha kuvaa namba hiyo.

CR7 ni brand ambayo hata ligi haitakuwa tayari kuizuia, kibiashara asipovaa namba 7 kuna vitu havitaenda sawa.
 
Kitu kikubwa ninachokitegemea ni kuwa vichezaji uchwara vilivyoshindwa kufanya mambo sasa vitaanza kuisoma namba na kuondoka..

It's high time kwa Ole kumwambia Martial hivi;

"Bwana mdogo si unaona mambo hayo ya CR7?,fanya kuondoka mapema tu"..

Same thing kwa James.

Rashford naye aambiwe his game time can only be secured kwa yeye kuperform consistently..mambo ya yeye kucheza kila siku huku akicheza ushubwada yameisha.

Na Ole aelewe kuwa ana kikosi bora kabisa cha kushinda kila kitu ulaya..no more excuses.


======

Henderson

Varane Maguire Shaw

Sancho Fred Fernandes Pogba

Rashford Cavani Ronaldo

========

Henderson

AWB Varane Maguire Shaw

Fernandes Fred Pogba

Greenwood Cavani Ronaldo

=========

GGMU
 
Tutakwenda na 4-4--2..

CR7 ...cavani 9


Rashford... Pogba Bruno. Sancho.

Shaw,magwea,varane bisaka.

Tutaachana na DM..

Kama ole yupo serious na makombe,..
No,.hauwezi chezesha Cavan na Ronaldo at pa. Fred, Tominay au Matic lazima mmoja awepo. Ronaldo/Rashid kushoto, Sancho kulia, Pogba 8,.Bruno 10, Cf Marson au Cavan.

Rashid
 
Mmesajiri jina (brand) lakini hakuna mchezaji sasa hivi pale

Ufanisi wake ulikua Madrid , ata kule juve hakufanya la maana zaidi ya watu hadi wakakosa kombe la ligi

Sasa hivi hakabi, yeye anakimbia na move tu
Muoga sana kuingia zile 50-50, anajua akipata majerui makubwa ndio basi tena

Haya mapambio ya mwanzo ila baada ya x-mass au 2022 kabisa tutaimba nyimbo ya aina moja
 
Sasa hivi tukitaka mchezaji ni simu moja tu hata yule Mbappe si idol wake tunaye tukimuita anasahau ndoto zake za kwenda Los Blancos.

Next season kituo cha kwanza ni Germany, Dortmund watupe mtu wetu. Kwa influence ya Sancho na Solskjaer na muundo wa kikosi chetu lolote linaweza kutokea.
 
Mmesajiri jina (brand) lakini hakuna mchezaji sasa hivi pale

Ufanisi wake ulikua Madrid , ata kule juve hakufanya la maana zaidi ya watu hadi wakakosa kombe la ligi

Sasa hivi hakabi, yeye anakimbia na move tu
Muoga sana kuingia zile 50-50, anajua akipata majerui makubwa ndio basi tena

Haya mapambio ya mwanzo ila baada ya x-mass au 2022 kabisa tutaimba nyimbo ya aina moja
Yani mtu wa miaka 36 unataka afanye aliyokuwa anafanya akiwa na miaka 20?

Ronaldo uwezo wa kufunga goli 20 kwa msimu anao na hilo ndiyo suala la msingi. MAUMIVU YAKIZIDI MUONE DAKTARI.
 
Back
Top Bottom