Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Hakuna kitu au jambo lolote lile chini ya dunia hii likakosa bahati, hata hao wazungu wenyewe wanajua hilo na wanaiita lucky, sisi tumekosa kujituma na bahati pia na ndiyo maana unakuta tunapigiana penalti 10 zote zinaingia ila yetu ya 11 tunakosa.
Huwezi kuwa na bahati bila kujituma.

Nimeuliza pale kuja kwa Ronaldo kutaongeza au kupunguza laissez faire attitude ya Ole ?
 
Huu usajili japo mzuri ila ni wa Kudandia
Man City walishajitoa ndio ninyi mkaingia
Man u hamkusahau dandia dandia kama hizi huko nyuma iliwacost
Sanchez alikuwa aende Man city ninyi mkapiku
Lukaku alikuwa aje Chelsea ninyi mkapiku

Cristiano Ronaldo katika umri huu bado anao uwezo mkubwa sana japo umeshuka sana
Swali ni je mlimuhitaji, jibu hapana, angekuwa Ronaldo ni mdogo wa miaka 20-25 tungesema alihitajika kwa ujenzi wa timu wa muda mrefu
Pamoaj na kuwa CR7 hakuhitaji je bado atawafaa, jibu ni yes, bado Ronaldo ana uwezo wa kufunga goli 20 kitu ambayo hakuna winga hata mmoja wa sasa mwenye uwezo huo
Madhara yake makubwa ni overload ya mshahara
 
Halaand inasemekana psg
 
Jombaa, Ktk dirisha tulilowahi kufanya vizuri basi hili lipo very strategic nina uhakika Cristiano Ronaldo tumemchukua ili kuongeza hali kujiamini kikosini.

Vichezaji vya hovyo sasa ni muda muafaka kufagia nyumba. Tunataka heshima yetu irejee tumevivumilia sana vichezaji vya hovyo.

Pale mbele Ed, Cristiano, Mason na Bruno wengine wote waji-prove kwa nini wapewe nafasi.

Furaha niliyonayo hapa haina kifani. Ni kweli tunahitaji kiungo wa ulinzi ila bado tulihitaji mtu mbele aliye serious ili aje kutusaidia kuondoa vichezaji vya hovyo tulivyovijaza pale.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…