ze-dudu
JF-Expert Member
- Jul 26, 2014
- 18,428
- 24,145
Nilishaandika humu mdau jamaa asepe tu maana kama timu kashaijenga ipasavyo huyo atakaekuja ni kuongezea mambo mawili matatu makombe yaanze kumiminika.......Msimu umeisha rasmi jumatano wacha tuteme vinyongo vyetu.
The end justify the means.
Ole hajabeba walau kombe hata moja la kuzugia na mbaya zaidi alikuwa anatolewa na timu zisizotarajiwa kwenye mashindano mbalimbali.
Kwenye FA tumetolewa na leicester ya Brendan Rogers ambaye liverpool walimfukuza baada ya project yake kufeli pale anfield.
Europa kashindwa kuchukua ndoo dhidi ya villareal ya Unai Emery aliyeshindwa kufanya kitu na arsenal pale emirates.
Champions League kashindwa kupata matokeo sahihi dhidi ya waturuki na kahitimishiwa safari na Leipzig ilhali alikuwa ameishatanguliza mguu mmoja ndani ya 16 bora. Sina kumbukumbu sahihi kuhusu carabao alitolewa na nani.
Miaka 3 ni mingi sana kwa kocha sahihi kuonyesha mwelekeo wa timu kama united katika kugombania makombe makubwa na madogo. Kwa walio wengi wanaamini Ole ni mtu sahihi kwa united sababu amerudisha utulivu ndani ya dressing room iliyovurugwa na Pogba (ugomvi wake na mourinho). Binafsi kama ambavyo nimekuwa nikipinga uwepo wake united,sababu kubwa anapungukiwa mbinu dhidi ya makocha wanaofundisha timu tunazoziita midtable ila ana kismarti na timu za top 6. Hii inatoa tafsiri kuwa ana staili moja tu ya ushindi (low blocks kama anavyoisemea mkuu Daemusin ). Bruno amekuwa akichagiza matokeo ya ushindi kwa united kwa kiasi kikubwa nadhani kuliko Ole mwenyewe ndio maana hata mechi ndogo tu za mchangani akikosekana yeye unaona tunacheza mpira usiokua na malengo kabisa. Kwenye mashindano ya carabao,fa,epl,europa na champion league mbinu hubadilika kutokana na mpinzani unayekabiliana naye,hatua uliyopo na hata muda wa ligi unaokuwa umebaki,lakini mbinu pamoja na mifumo ya Ole imebaki ile ile kila siku na kila mechi kwa kila mpinzani.
Sababu ya pili kwa nini Ole si mtu sahihi kwa united ni uoga wake wa kufanya maaamuzi kabla na wakati wa mechi. Tumekuwa tukiona marudio ya makosa ya wachezaji wa kiingereza ndani ya united lakini watalazimishwa kumaliza mechi hivyo hivyo au mechi inayofuata wataanza kama kawaida. Kama rashford alivyomaliza msimu akiwa kwenye kiwango cha chini,ndivyo ambavyo tuliona maguire akilazimishwa kucheza game after game kipindi akiwa hana kiwango cha kuridhisha.
Mwaka 2013 zambia walifuzu kucheza kombe la mataifa huru ya afrika wakiwa chini ya kocha ambaye chama cha soka cha zambia hakikuridhishwa na mbinu pamoja na mifumo yake hivyo wakamtema na kumchukua renee mfaransa ambaye alifikia kuwapa kombe mwaka huo. Hivyo natoa rai tuachane na Ole maana kwa hapa alipotufikisha inatosha hivyo tumtafute kocha atakayeweza kutuvusha hatua hii tuliyokwama na babyface assassin wetu.
ze-dudu
Rejea madrid ya zidane ilisukwa na carlo mou yeye kaja kujibebea trebble uefa kilaiiini......


These five Reds racked up the appearances in 2020/21 ★

★
— Jorge Mendes has given the prospect of moving Cristiano Ronaldo back to #mufc a good go & a good amount of thought. He's had contact with the club, who'd gladly welcome him back, but cannot afford such an expensive operation [Sport Witness]★
️
★