Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Hivi mechi na Liverpool itachezeka lini?

Hii ni ratiba ya timu zote mbili.

May, 6 Roma vs United - EL

May, 8 L'pool vs Soton - PL

May, 9 Aston Villa vs United - PL

May, 12 United vs Leicester - PL

May,16 West Brom vs L'pool - PL

May, 19 United vs Fulham
Burnley vs L'pool

May, 23 L'pool vs Palace
Wolves vs United

May, 26 EL final

* PL - Premier league
EL - Europa league
nyumbu akili hamna

Sent from my SM-J200H using JamiiForums mobile app
 
Man Utd have given Glazers more money than the actual amount they spent on transfers.

£1.07bn vs £1.01bn
IMG_20210504_145042.jpg
 
Liverpool apewe point 3 tu ,sababu mliogopa kuingia uwanjan mkajifanya mnaharibu uwanja

Kuku nyie
 
kumekucha jamani

José Mourinho is the new AS Roma manager. He has signed until June 2024. Maurizio Sarri has never been an option
Hivi Jose bado anataka kuthibitisha nini kwenye ulimwengu wa soka baada ya mafanikio aliyokwisha yapata?
Kimbinu,namuona kama hana jipya baada ya kuibuka kwa kundi la mameneja wengi vijana wanaofundisha soka la mbinu pamoja na burudani.
Kama ilivyo kwa Pep,nguvu kubwa ya Mou iko katika matumizi makubwa ya pesa ili kutengeneza timu ya ushindani. Kwa Roma hii pamoja na vilabu vingi vya serie A,kwa sasa uchumi wao hauwezi kumbeba kufanikisha hilo.
Kwa sasa uchambuzi ungemfaa zaidi.
 
pande zote mbili zinahitajiana kwa dhumuni la kurudishiana heshima iliokwisha potea, As roma na wamiliki wao bila ya shaka
walihitaji kocha mwenye uzoefu atakayewafanya waongelewe zaidi kama walivyo wapinzani wao wakuu na bahati nzuri jose ni target sahihi kwao.

Soka la Italy kwa sasa linamfaa zaidi jose kutokana na ukosefu wa ushindani hususani eneo la bajeti ya usajili kwa vilabu vingi (naamini kama watampa fedha ya kuimarisha timu japo kwa madirisha mawili anaweza kuwapa faida kubwa sana), faida nyengine kwake ni ufinyu wa makocha waliosonga mbele zaidi kimbinu ukilinganisha na premier league.

Anachopaswa kufanya jose ni kurekebisha mfumo wake wa usimamizi na uongozaji wa timu, ni muda muafaka sasa na yeye akubali kubeba mzigo wa lawama kama wafanyavyo wenzake pindi mambo yanapokwenda mrama.

jose amekuwa ni bingwa wa kuangushia wachezaji na uongozi shutuma, mara zote anaibuka mshindi wa ligi ya utakatifu na usafi
 
Back
Top Bottom