Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Watafanikiwa tu maana walishaanza na nation league

Halafu hii idea ingekuja africa aisee
 
Hata goli la 3 movement ya ule mpira kama angekuwepo Rashford au Martial lile goli lisingefungwa ungeona mjinga mmoja anafinya finya wakati watu wameishaji-position.
 
Hii superleague wanataka iweje?..tofauti na UCL?
Yes, Hii ni ajenda yenye msukumo wa tamaa ya kutaka kupiga pesa kutoka kwa wamarekani wanaomiliki vilabu vya Manchester United, Liverpool na Arsenal. Hili ndio genge lililo nyuma ya huu mpango. Anayenishangaza ni boss Juventus (Andrea Agnelli) naye yuko nyuma ya huu mpango na ni mjumbe wa bodi ya UEFA pia.

Ukisoma mpango wao unaonyesha utakuwa na timu 15 za kudumu kutoka ligi kubwa 5 barani ulaya. Na tayari makubaliano ya awali na siri wamefikia na vilabu vyote 15 na vitaanza kuthibitisha kuanzia jumapili ya leo.

Mfumo wake wa uchezaji utafanana na ule wa mpira wa kikapu (NBA) sio kama huu tuliouzoea wa kawaida yaani kutakuwa na timu 15 za kudumu halafu 5 zitaingia kwa mfumo wa kushindania jumla watakuwa na timu 20. Zitatengwa kwa makundi mawili kila kundi timu 10. Washindi wanne wa juu ktk kila kundi watasonga mbele. Mechi zitakuwa zinachezeka katikati ya wiki na fainali itachezwa weekend baada hatua zote kuisha.

Timu zilizo ktk orodha ni Manchester United, Arsenal, Liverpool, Chelsea, Tottenham, Manchester City, Barcelona, Real Madrid, Bayern Munich, Juventus, Inter Milan, AC Milan, PSG, Atletico Madrid na Borussia Dortmund.

Mpaka kufikia leo ni PSG tu ndio aliyegoma kabisa kufanya makubaliano ya awali bosi wao (Nasser al-Khelaifi) ni mjumbe wa UEFA na pia ni mtendaji mkuu wa beIN Media Group hawa wanamiliki haki za kurusha matangazo ya UEFA kwa hiyo maslai yake yanaguswa.

Business proposal ya hii super league inaonyesha watakuwa wanaingiza €4B kwa mwaka kupitia matangazo mara mbili ya kiasi wanachotengeneza UEFA kwa sasa ( 2018/2019 walipata €2.4B). Vilabu huku vitakuwa vinalamba mpunga mara mbili ya wanaoupata sasa.

Mwenyekiti wa hii super league atakuwa Florentino Perez (Real Madrid) makamu watakuwa wanne Joel Glazer (Manchester United), John W. Henry (Liverpool), Stan Kraonke (Arsenal) na Andrea Agnelli (Juventus).

Hata hivyo vyama vingi vya soka vinapingana na agenda ya hawa wamarekani wakiwemo waingereza na wajerumani. Inaomekana hawatatoa vibali kwa vilabu kushiriki huko.
 
Siku zote huwa nasema Maguire huwa anafanya makosa mengi ya kijinga sana kuliko Lindelof.
 
Naona hashtags nyingi sana huko mitandaoni zinatembea, #Say no to Super cup.
 


sitaki kuamini ya kwamba hawa jamaa wamefikia uamuzi wakiwa peke yao, bila ya shaka kuna kundi kubwa la wafanya biashara, vyombo vya habari vikubwa vipo nyuma ya mkakati huu.

ngoja tuendeleee kuishuhudia hii vita kati ya matajiri na wazee wa kusimamia kanuni, sheria, miongozo na taratibu za soka ulimwenguni.

kwa waliofatilia hili sakata nahitaji kufahamu mfumo wa ligi utakuwaje ndani ya uwanja, niliwahi kusikia nyakati za mwanzoni kabisa ya kwamba hii ligi itachezwa viwanja tofauti vya nchi kama vile marekani na nchi za kiarabu, china. Lengo kuu ni kuwapa nafasi mashabiki wa nchi tofauti kuzishuhudia team wazipendazo

Je kuna ukweli wowote,
Chief-Mkwawa na Joh Doe
 
[Swiss Ramble] - Here's a clue as to why 12 clubs have signed up for a European Super League: They lost a combined £1.2 billion in 2019/20 before player sales*. And that was for a season where only the last 3 months were impacted by COVID... *Liverpool have not yet published their accounts
 
Marekani kautafuta sana mpira wa miguu kipindi cha Blatter, kaukosa.

Sasa hivi wanakuja kivingine.

Ukitaka kujua ita operate vipi Angalia ligi ya NFL Marekani, huko ndio Kina Glazer walipoanzia, ligi ambayo haina kushuka daraja, watu Wana cheza tu for fun basi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…