Kitoabu
JF-Expert Member
- Jul 7, 2011
- 11,080
- 12,319
Ukisemea hivyo, tutahitaji historia za timu hizo tangu kuanzishwa, nani anaongoza kumfunga mwenzie?Vipigo kwenu havijaanzia msimu huu pekee
Sina utundu wa kwenda kuyafukua makalabrasha, lakini naimani hata wewe unajua kua Arsenal kafungwa mala nyingi na man united kuliko yeye kumfunga.
Nyakati nimepagawa na Man united (1998 - 2013) Arsenal alikua hamfungi Man United, kwenye game 6 unaweza kuta Arsenal kashinda moja.
Tushawapigeni bao 6, tukawapasueni 8 (tena hii juzi tu hapa hata mwanangu wa kwanza keshazaliwa) izo bao nne nne ndio usiseme.
Namkumbuka kuna game Giggs alipiga chenga kijiji cha Arsenal kuanzi kati mpaka golini akapasia nyavu, nakumbuka ilikua FA Giggs akazawadiwa mchezaji bora wa mechi.
Mwisho wenu wa kuchukua ubingwa, nakumbuka mulichukua ubingwa bila kufungwa hata mechi moja, lakini hata hivyo sisi hamkuwahi kutufunga msimu ule , nakumbuka mulirudi tena kwa speed yenu ile ile msimu ulio fuata.
Muliwafunga vibonde wenzenu, lakini mulipo kutana na Man united mulipotea.
Nakumbuka alitupia Van Nesroy na Wayn Roon, tena King Roony ndio ilikua game yake ya kwanza kuichezea Man united dhidi ya Arsenal, Kama sikosei alitupia mbili siku ile.
Nahuo ndio ukawa mwisho wa Arsenal yenye kwenye mafanikio.
Kiufupi Arsenal ndio timu hasimu kwangu kwenye ligi ya EPL sababu kipindi naanza kushabikia soccer Chelsea ilikua na mashabiki wachache sana, Liverpool walipoteana (kama sisi miaka hii) hiyo taka taka Man city hakuna alie tegemea italeta maajabu.
Kwahiyo historia yetu ya miaka ya hapa kati (1998 - 2021) naijua vizuri.
Nyie mumeanza kuota mapembe juzi tu hapa misimu kama minne nyuma, ila chini ya Sorkskjaer naamini tuta yakata hayo mapembe yenu.
Ngoja tutengeneze kizazi cha kina Green wood na wenzake, tuna kuja.
Misimu mitatu mbele mengi tutarudi kwenye ubora wetu, maendeleo hayaji kama mwanga wa tochi.
