Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Akipunguza kutolewa kwenye nusu fainali atakuwa pia ametupigisha step kimtindo..
 
★Bruno Fernandes is only the third player in Europe's top five leagues to reach double figures for both goals and assists this season.

️ 14 goals
10 assists

What an impact


Bruno Fernandes has scored and assisted in a league game for the seventh time this season, more than any player across Europe's top five leagues this season★

#GGMU


manutd |
 
Mkuu Daemusin binafsi nilipenda kusitokee timu ikatawala epl kama anavyojaribu kufanya Mr Pep kwa sasa maana itaondoa kule kutokutabirika kwa bingwa wa ligi msimu hadi msimu.
Mtizamo wangu kama ilivyokuwa kwa wengi wasiopenda liverpool kuchukua kombe msimu ule ni kwa sababu ya kale kaheshima tulikobaki tunajivunia kwa sasa (bingwa wa kihistoria wa epl) maana tuko mbali sana na uwezekano wa kuchukua kombe mbele ya hawa watabe city and co. Hivyo,pamoja na utawala wa City chini ya Pep hata akusanye mara 10 bado hataweza kuivunja hii rekodi. Wakati huo huo kwa upande wa liverpool ni kinyume chake na tungekuwa yatima kwa kusimangwa humu na wale wajuaji.

Kwa upande mwingine Pep amebadili mwelekeo wa uwekezaji kwenye soka la uingereza hasa kwa vilabu vinavyowania mataji kwa nadharia mbili;
1. Kwa sasa kutengeneza wachezaji wa academy ni kwa ajili ya kuuza na kutunisha mfuko ili ununue galactico kwa ajili ya kujiimarisha zaidi.
Hivyo hii nayo inafanyika kwa minajili ya kibiashara zaidi kuliko kuiimarisha timu husika.
2. Waarabu wa city hawategemei faida itokanayo na mpira/klabu kujiongezea kipato bali kuitumia hii platform ya city kujitangaza na kufanikisha madili mengine muhimu zaidi ukilinganisha na wale wamarekani wa liverpool na united wanaotegemea kuvuna kutoka kwenye timu zao.


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…