Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Ni kweli ni individual error ndio zinatuangusha lakini kitendo cha kujirudia rudia kila mechi huoni naye anawajibika kwenye hilo mkuu?
Mfano mzuri goli la kwanza limetokana na ujinga wa maguire pamoja na de gea,lakini mechi ijayo watakuwa ndani tena kutugharimu hivi.
Ni kama OGS anakosa sauti kwa baadhi ya wachezaji ndio maana hii tabia huwa inajirudia rudia.
 
Usidanganyike na maneno ya umu JF, Dean Herderson bado hajaiva kukaa pale golini mkuu, ndio maana anazoeshwa taratibu na vimechi vya FA na Europer, Peter Schumeichel alishawai zungumzia hili ktk interview zake, alisema pressure ya kuwa mlinda mlango #1 Shielfied ni dunia tofaut na kuwa #1 OT

Kwa beki tulizonazo pale Carington hakuna wa kumuweka bechi Maguire pamoja na mapungufu yake

OGS anachofanya anatumia wachezaji alionao pa1 na kuwaboresha viwango vyao

Unasema una mashaka na OGS! Sawa nakuliza swali,

kabla msimu huu 2020/2021 haujanza uliwaza mpaka kufika leo Feb 07 tungekua nafasi tuliyopo ktk EPL Table??
 
Ila compared na Manchester United nani aliyepoteza nafasi nyingi za wazi?

Au ulitaka OGS aingie ndani akabe ile faulo ya last minutes?
Kocha anapaswa kufundisha timu yake jinsi ya kukaba/kuzuia , alipaswa kufanya sub ya kiungo mapema Everton walioneakana wanatawala katikati benchi kulikuwa na VDB & Matic hakukuwa na sababu kumuingiza Tuanzebe
 
Kocha anapaswa kufundisha timu yake jinsi ya kukaba/kuzuia , alipaswa kufanya sub ya kiungo mapema Everton walioneakana wanatawala katikati benchi kulikuwa na VDB & Matic hakukuwa na sababu kumuingiza Tuanzebe
Mpaka everton wanasawazisha ni sisi Machester tulikua tunatawala mchezo kuanzia kiungo mpaka kushambulia,

Tuanzebe kawa kafala kwasababu everton walisawazisha goli tofaut na hapo wala maneno yasingekuwepo, na baada ya faulo jukumu la kulinda ile faulo si ni la timu nzima?

Mara ngap uwa ananzishwa Matic washabik tunalalamika Matic yupo slow, mara ngap dogo VDB ananzishwa anazingua wakuu?

James Rodguez anapigiwa pass yupo alone ndani ya 18 anajiandaa ana'shoot uku Fred anamkaba kwa macho, ulitaka OGS aingie akabe? Na kumbuka huyu Fred kwa mechi zetu msimu huu kawa the best DM
 
Mkuu mozila firefox ,kwa kweli sikuwaza kama hata top 4 tungeingia endapo wapinzani wetu wangekuwa kwenye kiwango chao bora kabisa na bila majeruhi ya mara kwa mara kwenye vikosi vyao vya kwanza.
Lakini cha kushangaza msimu huu united chini ya ole ndio timu ambayo tunaona kama iko kwenye form nzuri na tukapata bahati ya kupitiwa mbali na majeruhi kwa key players wetu. Nami nikuulize swali dogo,OLe anakosa kipi kwa msimu huu kuwa title contender?
Tusitegemee liverpool,city,chelsea chini ya tuchel msimu ujao watakuwa na bahati mbaya kama msimu huu wakati sisi bado tunasubiri rashford akiitafuta form yake.
 
3 SHOTS ON TARGET,3 GOALS! Hapa tunaongelea ubora upi wa de gea dhidi ya henderson?
Huoni kuna haja ya kumjaribu hata huyo dean kama anaweza kuzuia walau shot moja kati ya hayo matatu?
 
Kuongoza mechi sio kutawala mechi ,kutawala game ni ku-neutralize threat za mpinzani wako baada ya kufungwa midfield ya Everton (Doucoure,Gomez & James ) ilikuwa inapambana kurudisha magoli na wawili ndio wamefunga magoli.Baada ya kurudisha magoli 2 it was clear Everton strength yao ilikuwa katikati kabla ya kufika dakika za 80 kocha angeongeza kiungo katikati kupunguza pressure ya Everton

Hakuna aliyesema Matic aanze game,Matic sio slow kucheza dakika 20 au 25 kwa age yake na hajachezeshwa muda mrefu
 
Hehehe timu inayoshuka daraja inasajili kocha aliyetoka kushusha timu daraja naona mnatunza utamaduni.

Wewe nilikwambia huyo arteta angepewa shefield united au cadif zinashuka vizur tu kama una wakina aubameyang,lacazatte,pepe na partey upo huku
Vipi kama angepewa cadif?

Yaani hao niliowataja wananunua ile cadif na chenj juu au molde huyo kocha wenu anahangaika balaa yaani had moyes ambae hajafanya usajir na aston villa washamkata gepu ina maana arsenal sio big 6 ni timu ya daraja la kati had muda huu mnapamban kujinasua kushuka daraja
 
Nilishawahi kuuliza humu anaejua ogs anapotupeleka aniambie sijawahi kupewa jibu hata siku moja....
 
Hehehe data za Villa kutotumia pesa umeokota kijiwe cha wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…