Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Game ni ngumu sijajua kama watakuwepo au lah .

Soton wanakikosi Chenye muunganiko mzuri sana kutokuwepo kwa hao viumbe hakutabadilisha chochote hasa ukizingatia timu yetu imekuwa ikicheza vile vile bila kubadilisha mfumo wala intensity hivyo nategemea same Ole's predictable lunacy.
usiku mwema brother, hii ya kwako ndio caption bora ya mwaka kuhusu man utd...short and clear.... kuna tetesi za kumtaka danny ings kwa dirisha lijalo, kiupande wako unamuonaje?
 
Kuna wadau wanasema timu yetu inacheza kwa uoga against big teams hasa ukizingatia matokeo yetu dhidi ya timu hizo siyo ya kuridhisha kabisa.

Binafsi nina maoni tofauti kidogo juu ya hilo.

Ukiangalia timu yetu msimu huu karibu mechi zote tunatumia mfumo wa 4 2 3 1 au 4 4 2 diamond dhidi ya timu zote kubwa na ndogo.

Msimu uliopita tulicheza 4 2 3 1 dhidi ya timu ndogo na 3 4 2 1 dhidi ya timu kubwa ukiondoa mechi ya Liverpool pale Anfield tuliyocheza karibu mifumo yote uwanjani katika vipindi tofauti tofauti.

Kwanini tumeshindwa kuzifunga timu kubwa tukiwa na timu bora kuliko msimu uliopita ?
Binafsi naona kuna sababu kadhaa.
1. Safu yetu ya ushambuliaji kutokuwa clinical sana msimu huu kuliko msimu uliopita msimu huu tumetengeneza chances nyingi za kufunga magoli lakini tunatumia chache sana kupata magoli ilihali msimu uliopita washambuliaji wetu walitumia nafasi chache sana kutupa matokeo kwa sababu wote walikuwa form pamoja na kukabiliwa na majeraha.

2. Msimu huu timu nyingi kubwa zinacheza kwa tahadhari kubwa sana against United kiasi cha kutokushambulia carelessly kama msimu uliopita unaweza kuona mechi zetu zote against top teams tumepata goalless draw isipokuwa mechi na Arsenal OT na mechi dhidi ya Tottenham OT zingine zote ni goalless draw.

3. Counter attacking football ya Ole kushindwa kufanya kazi hasa ukizingatia sababu zangu mbili hapo juu ambayo ndiyo iliyomuua Guardiola mechi tatu mfululizo, unaweza kuona Man city waliamua kucheza 4 2 3 1 against United OT, Arsenal walicheza mfumo ule ule, na hawakushambulia kwa kujiachia ili wadhibiti mikimbio ya washambuliaji wetu.

Je Ole anacheza kiuoga dhidi ya timu kubwa ?
Jibu ni hapana msimu huu Ole anacheza na timu kubwa kwa kujiamini zaidi kuliko msimu uliopita.

Unaweza kuona katika mechi zote kubwa Ole katumia 4 2 3 1 au 4 4 2 diamond tofauti na msimu uliopita ambao alitumia 3 4 2 1 au 4 3 2 1mifumo ambayo ni completely defensive ukilinganisha na 4 2 3 1 au 4 4 2.

Ukiangalia possession ya Ole katika big games msimu huu na uliopita inaonyesha wazi msimu huu umiliki wa mpira umeongezeka tofauti na msimu uliopita against big teams.

Hata ukiangalia attempts on goal au chances created against big teams msimu huu zimeongezeka kuliko msimu uliopita.

Tumeshindwa kuzifunga timu kubwa siyo kwa sababu ya uoga wa Ole bali kwa sababu ya kushuka kiwango kwa safu yetu ya ushambuliaji na sababu zingine nilizoorodhesha pale juu.

Nawasubiri Southampton .
1015569332-850x560.jpg
 
usiku mwema brother, hii ya kwako ndio caption bora ya mwaka kuhusu man utd...short and clear.... kuna tetesi za kumtaka danny ings kwa dirisha lijalo, kiupande wako unamuonaje?
Kwangu mimi sioni sababu ya United kuendelea kukusanya wachezaji bila kutafuta mbadala wa pattern ya uchezaji wa timu.

Timu yetu haina muunganiko mzuri kiuchezaji na kwa hakika inacheza vibaya sana kuliko timu zote za EPL.

Tatizo la uchezaji mbovu na kukosa muunganiko linatokana na careless and laissez Faire coaching.
 
Game ni ngumu sijajua kama watakuwepo au lah .

Soton wanakikosi Chenye muunganiko mzuri sana kutokuwepo kwa hao viumbe hakutabadilisha chochote hasa ukizingatia timu yetu imekuwa ikicheza vile vile bila kubadilisha mfumo wala intensity hivyo nategemea same Ole's predictable lunacy.
Kwa kikosi Cha leo ole amerudi kwenye basics ya 433 with Fred Scott na Bruno as a ten. Kwa kumbukumbu zangu hiyo patern haijawah muangusha.

Ili tucheze diamond kama hizi game za karbuni tulizocheza wale forwards na number 10 wanatakiwa wafunge but kwa Sasa bruno magoli yamepungua na hao watoto wawili wa mbele utoto mwingi

Leo tusubiri ushindi tu
 
Back
Top Bottom