Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

★Sergio Ramos has chosen Manchester United as his next destination. He won't renew with Real Madrid. Figures have already been discussed [€226,000 per week]..★

#elchiringuitotv

manutd |
IMG_20210202_122008_318.jpeg
 
Ni swala la muda tu.

Mechi zao 3 zijazo wataambuliA sare zote hawana uwezo wa kushinda hizo mechi.

Timu inafungwa na sheffield nyumbani kwao.sheffield mpaka sasa wameshinda mechi 2 tu kwenye ligi moja ya mechi walioshinda ni dhidi ya United.

Raundi ya pili hii kwa Manyumbu ni ngumu sana kutokana na ushindi waliopta raundi ya kwanza ulikuwa wa ujanja janja.ndio maana saizi mechi Za marudiano wanashindwa kuchukua point 3.
Kwahiyo hata Livakuku nae alifungwa kiujanja ujanja, sio?
 
man u ndo sisi tukifungwa tunashangilia na tukishinda tunashangilia
no coplain lazima tukubaliane na vipindi

mbona liverpool toka nazaliwa hawaja chukua kombe nimeowa ndo wamechukua kombeee
 
Kumbe wewe umeona ninachokiona. Hiyo manake Ole ni very average coach

Sent using Jamii Forums mobile app
Watanzania kila siku wakifungwa lawama humtupia kocha.
Ndio maana kila siku vilabu vyao vimekua vinabadili makocha utadhani chupi.

Sasa mpira wa kibongo tusiupeleke ulaya, Kule watu waliamka kitambo.

Manchester United imeshinda hapa, kila siku sifa zinakwenda kwa wachezaji, leo tumepoteza game moja na sare moja, tayari lawama anapewa kocha.

Twendeni nae mpaka mwisho wa msimu ndio tu tujue kua anafaa ama vipi.
 
Kuna watu wanachuki binafsi na Ole.
Timu inaposhinda wanakwambia juhudi za wachezaji na sio kocha, inapofanya vibaya kocha anaibuka...
Kama mmeamua kulaumu timu inapofanya vibaya, msifuni pia timu inapofanya vizuri.
Wengiwao huonekana humu pindi timu inapo fanya vibaya.

Inavyo onekana inawanoga sana taarifa za timu kuajili kocha mpya.
 
na wanao lalamika sio washabiki kindaki ndaki wa man u
ni mashabiki upara mashabiki kelele

pia wapo mashabiki jirani wa arsenal na chelsea na washabiki wazee wa liverpool ambao zamani walikuwaga kimya
sijui ujasiri huo wa 2020 wametoa wapi
 
Maajabu ya Bruno Manchester United ni balaa kubwa

SUNDAY JANUARY 31 2021

MANCHESTER, ENGLAND.

MWAKA mmoja umepita, Manchester United tangu walipoanza mchakato wa kurudi anga za juu katika soka, lakini ni baada ya mwokozi wao kutua.

Huyo ni Bruno Fernandes, aliyewasili Old Trafford akitokea Sporting Lisbon kwa ada ya Pauni 55 milioni na tangu wakati huo ni mwaka sasa.

Bruno Fernandes ndio chanzo cha tabasamu la mashabiki wa Man United kwa sasa, wakiwa kwenye mchuano wa kuwania ubingwa wa Ligi Kuu England chini ya kocha Ole Gunnar Solskjaer.

Kabla Fernandes hajatua, wiki moja nyuma Man United ilitoka kula kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Burnley na wakati huo, Solskjaer alikuwa kwenye hali mbaya na mashabiki walianza kupiga kelele afukuzwe.

Matokeo hayo yaliwafanya washike nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi, pointi 24 nyuma ya vinara wa wakati huo, Liverpool na matumaini yalikuwa hafifu sana kwamba mambo yatabadilika.

Lakini, baada ya kutua tu Fernandes, mambo yalibadilika.

Baada ya ujio wa Fernandes, Man United ilimaliza msimu kwenye nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi na kufika nusu fainali tatu.

Msimu huu, Fernandez ameendeleza makali yake na Man United kwa wakati huu ni moja ya timu zinazotajwa kwenye mbio za ubingwa wa ligi.



Tangu Fernandes atue Man United, hakuna mchezaji yeyote kwenye Ligi Kuu England aliyefunga mabao mengi kumzidi, akiwa amefunga mara 28 katika michuano yote. Hata straika mtupiaji, Harry Kane amefunga mara 26 tu ndani ya muda huo, huku Kevin De Bruyne pekee ndiye aliyemzidi Fernandes kwa asisti, 21 kwa 17.

Ndani ya muda huo, ukiacha mechi ya jana dhidi ya Arsenal, Fernandes ameichezea Man United mechi 34 kwenye Ligi Kuu England na chama lake limeshinda 21 kati ya hizo. Kabla ya ujio wake, mechi kama hizo 34, Man United ilikuwa imeshinda 12 tu.

Kwa kutazama mwaka mmoja wa Fernandes kwenye kikosi cha Man United na mchango wake, kocha Solskjaer amebaki kumwaga sifa tu.

Alisema: “Safi sana. Tangu siku ya kwanza aliyokuja ameamsha hamasa kubwa. Ni ingizo muhimu sana. Ni mtu mtulivu, anapiga sana kazi na nadhani kila mtu analiona hilo ndani ya uwanja.

Nimevutiwa na mwaka wake huu wa kwanza na nina imani ataendelea hivi kwa muda mrefu zaidi.”

Fernandes amebadili mengi kuhusu Man United kuanzia ndani ya uwanja hadi nje ambako kulikuwa na mashabiki ambao walikuwa wakiikosoa na kuisakama. Sasa kila kitu kimebadilika na mwepesi wa kukosoa wenzake wanapofanya makosa ya kijinga, mfano Victor Lindelof aliporuhusu Man United kufungwa bao la pili la kizembe kwenye nusu fainali ya Europa League dhidi ya Sevilla. Fernandes hakupenda na kuonyesha hasira zake hapohapo dhidi ya Lindelof. Anataka matokeo mazuri katika kila mechi na wachezaji wenzake wameanza kumwolewa vile Man United inavyopaswa kuwa.

Solskjaer alisema: “Anatazama kila mechi kwenye TV, hasa mechi kubwa. Ukimuuliza ulitazama mechi ya jana usiku? Yeye siku zote anaangalia mechi. Ataendelea kuwa hivi kwa maisha yake yote ya soka, nina uhakika.”

Screenshot_20210202-150930.jpg
[/b]
 
My prediction

Manutd 3-1 Southampton

Edson Cavani to score at any time in the second half

BTTS

O2.5

Possession

Manutd 58% - Southampton 42%

1H (1-0) Manutd

2H (2-1) Manutd

Manutd to win both halves
 
Back
Top Bottom