Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Goli la kwanza kwa kuwa yeye anatumia mikono na mpiga kichwa anatumia kichwa, alipaswa kuucheza ule mpira. Huwa ni mwoga/sio aggressive kwenye mipira ya juu ndani ya box

Pia, goli la pili alifanya very poor clearence, ni kama alimpasia adui...ambapo huo mpira ndio ukaja kuleta madhara
Zile goli hapaswi hata kulaumiwa
 
Yani saa nyingine inakera sana. Kweli sisi ni wa kufungwa nyumbani na Sheffield.

Hii si fedheha ya kufungulia mwaka. Sheff ambae ndani ya game 19 alikua na Point 5 .

Man U wamejua kutudhalilisha aisee


Kwa kweli nimeumia mnoo
Usiumie mkuu sana mkuu. Mechi bado nyingi naamini mtarudi nafasi ya kwanza tu
 
Yametimia
Sosha hajakaa kiubingwa kabisa yani mi naamini bahati ndio itambeba kuchukua ubingwa wa epl lakini si uwezo....
Nikizikumbuka nusu fainali nne anapoteza sina hamu nae kabisaaaaaa

Hapo kwenye kuongozwa na bahati ni kitu nakiona kwenye hizi mechi mbili tatu,japo kuna wale unaona wanajitahidi lakini 60% ya wachezaji wetu ni wa hovyo tu

Ni kawaida yetu kupoteza mechi ndogo ndogo kama hizi
 
Bao la pili dee gea alisharuka kwenye timing nzuri aliempoteza ni tuanzebe....
Bao la kwanza yoyote anafungwa
Pasi aliyompigia mchezaji wa Sheffield je?..De Gea jana kazingua big time
 
Martial hastahili kuwa mchezaji wa timu yetu
Na mwezi wa sita asipotafutiwa timu ya kwenda utakuwa ni upumbavu mtupu.

Fagia hizi takataka,then leta vitu vya maana kama Grealish hivi ambao watatupa dimension tofauti..
 
Napita tu. Nimeleta saalam toka Sheffield United. Naomba mzipokee wenyeji wa nyumba hii!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…