Ubingwa upo kwa timu ndogo ndogo ambazo ni nyingi. Hebu jaribu kufikiria Liverpool mpaka mzunguko wa kwanza unaisha hajafungwa na timu kubwa hata moja ( City - sare, United - sare, Arsenal - aliwafunga, Chelsea - aliwafunga) lakini tumemzidi alama sita na wote tuna michezo sawa 19.Kitu tulicho regress ni Big matches, tumedrop compare na msimu uliopita, draw zimekua nyingi sana.
Kosa kubwa linalofanyika na safu ya ufundi msimu huu wanaingia na mbinu za uoga dhidi ya timu kubwa mara nyingi Ole haiandai timu kushinda hata ukisikiliza mahojiano yake kabla ya mechi yanaonyesha wazi wazi anaingia kutafuta sare. Ile mechi ya Liverpool juzi alisema kabisa hatuwezi kuwa tunakaa nyuma muda wote, hii kauli ni wazi aliingia kutafuta sare zaidi japokuwa tulikuwa tunaweza kuwafunga bila shida kabisa.
★

