Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Mechi ya Jana Ole alijikosesha ushindi mwenyewe kwa kuwaheshimu Liverpool kupita kiasi.

Sikuona sababu yoyote ya Ole kucheza 4 4 2 diamond & 4 5 1 kwenye mechi ya jana.

Kilichoshangaza zaidi ni Rashford kuanza kama lone Striker halafu Martial akacheza left wing.

Kumuanzisha Pogba kwenye right wing kulimrahishia kazi sana Andy Robertson that's why alikuwa anapanda sana kwani right wing haikuwa na threat yoyote.

Bruno Fernandes alikuwa amechoka sana na probably anahitaji kupumzika walau 3 consecutive games au apunguziwe dakika za kucheza.

Mechi ya jana tungeshinda kama Solkjaer angeanza na Greenwood/James kulia kisha kushoto acheze Rashford striker angecheza yoyote Cavani or Martial.
 
Afanye hivi jumapili ktk FA Cup, kulia amuanzishe Greenward au James, then kushoto acheze Rashford
 
Jana midfield yetu hasa first half haikuwa na lolote la maana kiasi cha kushindwa kutengeneza clear chances compared to Liverpool.

Second half tulijitahidi kuamka lakini bado tulikosa killer instincts hasa kwenye mechi ambayo scoring chances unazipata kwenye breaks tu.

Hakukuwa na sababu ya kutafuta draw Anfield dhidi ya Liverpool ambayo defence yake yote iko kitandani.

Upande dhaifu wa Liverpool defensively ni kulia kwao hivyo kuweka Rashford kule ingewafanya Fabinho na Mwenzake waelekeze nguvu kushoto kwetu at the same time ingemforce Thiago or Shaqir kushuka chini Bruno would have been freed from pressure.
 
Bado nafasi yetu ya kuongoza ligi iko palepale but pressure imeongezeka baada ya Man city kuamka kutoka usingizini.

Tunapaswa kushinda mechi zetu zote dhidi ya weaker teams hasa ukizingatia next round fixture yetu against big six mechi nyingi tutazicheza away vinginevyo tutarudi nafasi za chini tena.
 
huenda ni sura ya chadwick na meno yake yalikuwa ni chukizo kwake. Chadwick alinyimwa mpaka kipaji cha soka
Ila Hela mkuu zisikie tu, Chadwick ni Handsome sasa hivi, kama hujamshuhudia live akicheza Huwezi kua mini ukimuona leo.


Na pia Career yake sio mbaya, timu ndogo ndogo kina westham, reading, Burnley, Norwich etc kacheza sana huko.
 
Mbona kabadilika hivi!
Ila Hela mkuu zisikie tu, Chadwick ni Handsome sasa hivi, kama hujamshuhudia live akicheza Huwezi kua mini ukimuona leo.


Na pia Career yake sio mbaya, timu ndogo ndogo kina westham, reading, Burnley, Norwich etc kacheza sana huko.
 
1. Yanga
2. Simba

Dar es Salaam
 
Ulianza vizuri pale uliposema tatizo ni midfield. Huwezi kushinda mechi kama ball possession ni 36%. Hatukuweza kumiliki hata pasi nne za uhakika kipindi cha kwanza. Kwa hiyo hata Greenwood angeanza wa kumpatia mpira hangemwona. Mechi ya Fulham ampumzishe Fernandez kachoka ili awe fresh dhidi ya Liverpool FA jumapili.

Bila kutawala mpira kipindi cha kwanza ndiyo mtihani. Fred na MacTominay ni dhaifu. Mbele ya safari usajili wa Grealish na Maddison haukwepeki.
 
I think game plan aliyoingia OGS ilikuwa OK kosa lilikuwa kuanza na Martial badala ya Cavani ,Martial alipaswa kuingia sub angekuwa na impact kuliko alivyoanza.Mashambulizi ya Liverpool yanaanzia kwenye full back (Trent & Robertson) na jana wote walibanwa Mane na Salah hawakuwa na impact yeyote .Cavani ambaye ni natural stiker angewasumbua sana Liverpool CB (Fabinho & Henderson) hawakuwa na pressure yeyote

Mechi kama hizi huhitaji kupata nafasi 7 ndio ushinde nafasi tulizopata zilitosha kabisa kufunga magoli tatizo ni wachezaji wetu wanachelewa kufanya right decision kwenye right time.

Perfomance yetu against big team ndio inatuangusha kwenye game 5 tumefunga goli 1 tena la penati next round mambo yasipobadilika hali itakuwa ngumu
 
Bado natafakari inakuwaje tuwe na takwimu hizi za kipuuzi khalafu tutegemee tushinde mechi

Offside 8 wakati Liverpool 1 - Martial na Rashford ndiyo Offside zote hizi zinawahusu.

Ball possession 34% wakati Liverpool 66%

Goal attempts 8 wakati Liverpool 17

Completed passes 344 wakati Liverpool 677

Rashford kulimwa yellow dakika ya 84 ya majeruhi ni dalili alikuwa na msongo wa mawazo wa mpira kumkataa hata free kick alishindwa kuvuka ukuta wa Liverpool...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…