This time huenda tukamwadhibu Danny Ings hatakuwepo na Redmond pia.
Huyu Redmond ni msumbufu sana na hachoki kukimbia threat nyingine ni Che Adam' pamoja na Ward Prowse.
southampton wana apply pressing wakiwa juu, kivyovyote tunahitaji umakini mkubwa sana pindi tunapoanzisha mashambulizi yetu kuanzia nyuma na hapa walengwa wakuu wanaopaswa kuwa makini zaidi ni fred, pogba na hata donny (jamaa ni mlaini sana kama ulimuangalia vizuri mechi ya juzi) kama si speed ya southampton basi ningelikuwa mwalimu ningelianza na nemanja matic na fred pale chini.
fred na pogba hawachelewi kufanya tackling pindi wanaposhindwa kuposess mpira kwenye miguu yao na ile pressing ya wale wahuni ndio huzidi kuniongezea presha, tujihadhari sana na mipira ya adhabu na corner za bwana
ward prowse.
licha ya kukosekana kwa
danny ings tusisahau
Che Adams ana rekodi nzuri sana ya kuzifunga timu kubwa tokea msimu uliopita pamoja na yule obafemi.
romeu ni mchezaji rafu asiyeimbwa, unajua timu nyingi zinazo pressing hucheza rafu sana kwa dhumuni la kuharibu mipango ya adui pindi wanapo poteza mpira au kudhibitiwa kwa kuhofia counter attack za mara kwa mara.
tunamuhitaji
donny kuvunja pressing na tempo ya wale jamaa, donny ni hodari sana kwa pasi za haraka jambo linalopelekea pawepo na transition ya kiuchezaji kwa angles tofauti za uwanja(si aina ya mchezaji anayeangalia upande mmoja), ni uamuzi wa mwalimu kucheza kamari hapo kesho kutwa
kama ni jino kwa jino pale kati (scott vs fred)
jino kidogo na ufundi japo tunakuwa dhaifu kiulinzi (fred vs donny).
kimbia, kimbia,kimbia ndio silaha yetu itakayoweza kutuokoa tukiachana na bahati na uzembe wa adui na ili tukimbie pale mbele na beki zao zikimbie (tuvunje low blocks) tunamuhitaji cavani na si martial.
Tusisahau tuombee uzima wa wan bissaka kwa dhumuni la kumdhibiti bertrand ndipo tumfikirie redmond.
huyu mpuuzi naye ana balaa kule upande wa kulia, anaitwa
Kyle Walker-Peters
===============
hii ratiba ya mwezi December imejaa mitego
- tumeshinda mechi 7 ugenini za premier league ukichukua na za msimu uliopita lakini hatujawahi kushinda mechi 8 ugenini mfululizo, sijui tutaondoa hii laana?