Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Issue ni kwamba Hatuna Rw sasa hivi, aka hatuna muda wa kulea mtu. Angekuja hata Mtu kwa mkopo kwanza tukiwa tunaendelea kulea ama kumsubiri Sancho.

Uchezaji wetu tupo predictable sana sababu ya mashambulizi yetu yanajulikana


Ukiangalia hapo Fernandez, Martial, Rashford na matic wote wanacheza sana Kushoto, kati ya midfield/striker 6 wanne wanapitia kushoto, waliobakia wawili pogba na greenwood wamewekwa tu ili mradi kusikose mtu. Pogba Natural naye ni wa kushoto anacheza tu kulia na greenwood tunajua ni Striker, ukiangalia vibox vya pasi juu kulia ni almost watu hawafiki kabisa.

Tukiwa na Rw wa ukweli kwanza Kiwango cha Bissaka kitakuwa sana, pia timu itakuwa dynamic pande zote mbili zinashambulia.
 
Becks ni one of our own, kakulia pale pale Utd, na alivyoanza kufanya biashara akagombana na Fergie akauzwa Madrid.

Zamani tulikuwa na wachezaji wana Sura ngumu hao, kina Sheringham, Chadwick, stam, Keane etc
 
Kwa hio Ole kamshusha kiwango Dani James? You guys are not serious aisee, yaani Kamtoa mchezaji jalalani huko na kumleta kwenye Timu kubwa kama United na kumpa Nafasi leo unasema ameshushwa kiwango? Dani James ni Dani James uwezo wake ni kujituma na mbio, anafanya vizuri mechi kubwa ambapo kuna nafasi kuliko mechi ndogo watu wakipanga basi. Toka msimu uliopita yupo hivyo hivyo.

Na Traore na James ni mbingu na Ardhi, uchezaji wa traore anafananishwa na Messi, anaweza chukua kijiji, ana close control, ana jicho la pasi na Goli etc, sababu ana individual skills nyingi basi kwake linaweza lisiwe shida sana.

Bruno huyu huyu mwenye Goli na assist sawa na mechi alizocheza ameshuka kiwango?

Hakuna mchezaji Hata mmoja alieshuka Kiwango, ni fitness issues tu na mambo yatabadilika kadri tunavyokwenda mbele kwenye ligi.
 
Vile unaongea utadhani mpira unachezwa chumbani na muangaliaji ni ww pekeako.
 
So mechi 3 ni kigezo cha kumuangalia kocha na viwango vya mchezaji kwa timu ambayo hata pre season haijafanya? Wachezaji hata pamoja hawaja train?
Hao wengine kina Everton wamecheza mechi 10 au? Wachezaji aliowasajili Ole karibia wote wameshuka viwango japo wakati wanakuja walikuwa
Bissaka, DJ, Maguire, Fernandes we huoni? Je hao wote amecheza nao mechi 3?
 
Hao wengine kina Everton wamecheza mechi 10 au? Wachezaji aliowasajili Ole karibia wote wameshuka viwango japo wakati wanakuja walikuwa
Bissaka, DJ, Maguire, Fernandes we huoni? Je hao wote amecheza nao mechi 3?
Bissaka mechi ya kwanza yenyewe ya palace hakuwa fit na hajacheza amecheza mechi 2 tu.

Tatizo lenu nyie mnajua mpira ni playstation unawasha tu kwenye umeme na kuanza kucheza, fitness ni jambo muhimu sana tena sana.

Angalia wote ambao wapo juu Epl hawajacheza michuano ya Ulaya, hii ni training regime ya Everton kabla ya Epl
Full Practice Game Part Of Everton's Training Plan For League Restart
Report: 19-year-old prospect has been in Everton first-team training ever since they returned – HITC

Sisi wachezaji wamekutana mechi ya palace ya ligi, hata mechi ya kirafiki ya Villa kikosi cha kwanza kilikuwa hakija report

Niliwahi kuandika matokeo ya timu zilizofika mbali ulaya, bayern mechi 2 zilizopita karuhusu goli 7, lyon ana Mechi ya 5 mfululizo hajui ushindi, sio coincidence hii.

Trust me timu yetu inapo regain fitness utaona na ushindi mfululizo unavyokuja, bado nina imani mwaka huuu tunachallenge Epl ubingwa.
 
Katika hayo magoli penati ngapi?
 
Ni kweli wachezaji man u hawapofit lkn je nani anayepaswa kuhakikisha fitness ya kikosi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…