Mkuu
Bavaria mie nakuunga mikono na miguu kwenye hii kampeni yako ya #Oleout ingawa huisemi moja kwa moja bali unajaribu kuwaonyesha watu kwa mifano kabisa.
Mfano upi?
Niligundua ubovu wa Ole msimu uliopita.
Mchezo anaoucheza ni mbaya kuliko hata enzi za Mou.
Wachezaji ukiwaona wamepungua viwango kuliko maelezo.
Msimu uliopita Bruno aliibeba United mgongoni, tukasema angekuja toka mwanzo wa msimu tungeongea habari za kubeba kombe.
Ghafla msimu huu amekuwa kimeo, akaletwa VDB.
Kumkosa Sancho isiwe sababu ya sisi kufanya vibaya hivi.
Kocha mwenye uwezo lazima awe na mbinu mbadala kucheza bila kutegemea RW.
Bissaka leo ameonekana mbovu, kwahiyo anatakiwa aletwe mwingine kuziba nafasi yake.
Lindelof alocheza vizuri wakati wa Mou, leo anaonekana mbovu. Anatakiwa aje mwingine wa ku-pair vizuri na Maguire.
Unamuuza namba 9 mzuri kama Lukaku, tena unajiamini kabisa kuwa Martial anatosha. Leo kiko wapi?
Rashford amebaki kulamba midomo tu. Chief-Mkwawa anakwambia bado jamaa ni 'mtoto'.
Lingard alicheza vizuri wakati wa Mou, leo hii unaambiwa hafai.
Nadhani ni mimi peke angu ndo naona Man Utd tunacheza mpira mbaya sana. Vipasi vya kijingajinga tunapiga.
Eti leo tunasherekea kuja kwa kizee kama Cavan, wapi Ighalo? Ole ameshindwa mtumia? Au hafit kwenye mfumo?
Ole ana mfumo? Miaka nenda rudi anatumia mfumo uleule kila siku na unamshinda. Hana game plan.
Hata wakija makocha 100. Kama kocha hafai aoneshwe pa kutokea.
Au tuandamane mashabiki waondoke Glazers na Ed wao ndo timu ianze upya. Otherwise, tufukuze tu makocha mpaka yule atakaeweza tumia resources alizonazo.