Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Timu itabadilika mazee msikate tamaa kwa kipigo cha jana uzuri kila mchezaji ashatoa ya moyoni na majuto kuhusu jana
1601847668534.jpg
 
Leo naona tetesi nyingi za Man Utd.
hii hali iliwakuta arsenal msimu ule waliofungwa magoli 8 na man utd.
==========
hatujui kinachoendelea huko ndani ila kwa jicho la kawaida unagundua ya kwamba ed woodward bado amekuwa akihangaika kuhakikisha ya kwamba anatimiza takwa la mwalimu kwa kumletea mchezaji husika na ndivyo ninavyojiaminisha(ed woodward hawezi kuitakia mabaya man utd)

changamoto inakuja pale ambapo muuzaji lengwa anaposhindwa kukubaliana na ombi la mnunuaji (bei ya kuuza mchezaji), hapo ndio tunajikuta tunapoteza muda mwingi sana kufanya mazungumzo yatakayowezesha pande zote zinafanya biashara itakayowafaidisha pande zote (tunasahau kwenye negotiation mwenye nguvu anakuwa ni muuzaji labda itokezee awe na shida kubwa sana yenye kuambatana ubinadamu wa kibiashara)

ukiagalia situation ya usajili wa sancho tokea mapema ilishaonyesha ni upi muelekeo wa dortmund (mpaka leo hii msimamo wao umebaki vile vile kwa kutokuwa tayari kumuuza mchezaji chini ya kiwango walichokiweka), unajiuliza ni kipi kinachotufanya kupoteza muda mwingi haliyakuwa hatuna uwezo wa kufikia thamani iliowekwa na pia hatuna uwezo wa kuwashawishi dortmund kumuuza mchezaji kwa thamani tunayoihitaji (ina maana tokea mapema tulipaswa kuangalia alternative nyenginezo)

kama mwalimu hakuwa na second option basi hilo ni tatizo lake na kwa solskjaer nina wasiwasi huenda hakuwa na target nyengine kwa winga wa kulia baada ya sancho ndio maana tumekuwa wapapatikaji ( leo bale, kesho doglas costa, keshokutwa dembele, na hao wote huko kwao hawatakiwi basi ingelikuwa ni rahisi kukamilisha sajili zao).

ila kama mwalimu aliidhinisha second option kwa kila target lengwa lakini bado bodi ikashindwa kufanya kazi yake kwa usahihi kwa takribani miezi mitatu ndio tutakuwa tunarudi palepale kwenye kesi yetu ya kila siku (tuna wasimamamizi wabovu).
 
Alikuwa timu ya vijana senior team amecheza dakika 86
mbona jamaa wanataka tuwape euro millioni 30 na nyongeza juu kwa mchezaji wa dakika 90.
usajili wake unakamilika rasmi january 2021 kwa mujibu wa dimarzio na fabrizio romano.

hii pesa tuliowapa ni kubwa sana kwa mchezaji asiyekuwa na uzoefu wa timu kubwa labda pengine tumeona dogo ana maajabu ya messi na ronaldo
 
Back
Top Bottom