chilubi,
Unakosa kutizima taswira pana zaidi ya uhalisia, timu nzuri hujengwa kwa zaidi ya matumizi ya pesa nyingi, pesa ni moja ya variable tu ktk the whole equation. Unamfahamu mtu mwenye majukumu ya kuajiri kocha wa Manchester United? Mtu mwenye majukumu wa kuajiri watafuta vipaji wa timu? Hujakosea ubashiri wako, ni Ed Woodward. Mpaka sasa tumeshaajiri makocha zaidi ya 5 chini ya Ed na wawili ni manguli wameshinda mataji ya kila aina kwa ujumla wao wana mataji zaidi ya 50 (Jose & LVG), bado tu unaamini ni coaaching area ndio pana upungufu? Ni kweli Ole ni average ila nani amemuajiri Ole?
Kuweka kumbu kumbu sawa, sisi Manchester United ndio tumetumia pesa nyingi sana kwa miaka 7 toka Ed awe bosi mkuu kuliko timu yoyote pale Uingereza tumewazidi mpaka Manchester City. Timu nzuri hujengwa na combination ya smart talents from football executive to recruitment teams hata uwe na pesa kama za Jeff Bezos usipokuwa na watu smart hasa hasa wale ma-chief strategist ni kazi bure. Hujiulizi kwa nini timu kama Liverpool wanafanya vizuri ila hawatumii kuliko sisi? Kuna watu behind the scenes wanafanya kazi kile tunachoona sisi mashabiki uwanjani ni product ya mwisho kabisa baada ya kuwa na smart chief stategist (football executive) anaajiri watu sahihi ktk kila idara kuanzia coaching staffs, recruitment staffs & negotiators. Hivyo vyote vikiwa sawa hata uwanjani panakuwa sawa. Fanya simple observation Manchester United chini ya Peter Kenyon (1997 - 2002, huyu ndiye aliyeijenga Chelsea pia, 2003 - 2009) Vs David Gill (2003 - 2013) Vs Ed Woodward (2013 - up to date).
Ni zaidi ya pesa ili uweze kujenga timu nzuri, kitu kikubwa kuliko vyote unahitaji kuwa na very smart football executive hao wengine wote wanaajiriwa na huyu mtu. Ukiwa na huyu mtu kilaza hata ulete malaika awe kocha mkuu timu itafanya hovyo tu maana hapatakuwa na technical coordination nzuri.