Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Man U
Screenshot_20200920-084251.jpeg
 
NI MECHI YA KWANZA NA MSIMU NI KAMA UMEISHA..

Unajua muda mwingine tuwe wakweli kabisa.."HII KAZI NI KUBWA KWA OLE"..Ole ana matatizo kibao na kimbinu hajaweza kutufanya tuonekana kama ile United tuliyoizoea ikiwa kwenye ubora wake kipindi cha Fergie..Good thing ni kwamba huu msimu hamna kisingizio,,timu inajipigia vipasi uchwara tu muda wote

°°°Kuna watu wanasema hatuna timu kabisa[Who do you want to add in that squad to beat Palace?,Lewandowski?],hakuna krosi za maana zilizopigwa au nafasi kali zilizotengenezwa na viungo hata ukiwa na world class straika bado atapoteana...Too predictable


Sikatai tunahitaji;

✓RW
✓CB
✓Straika
✓LB Backup

Lakini bado kwa kikosi tulichonacho ilibidi lipigwe mbungi la kueleweka..Arsenal wanacheza pattern zinaonekana kabisa,sisi tumeshindwaje?..Arsenal wana kikosi bora kutushinda?

"""Ole kapoteza nusu fainali tatu kwa msimu mmoja,na kashindwa kabisa ku-manage gemu ndogo tu zenye tension"""This worry me

==============

Tuongee kuhusu hawa wachezaji;

Scott McTominay===Hatakuwa mchezaji bora kwetu ni mchezaji mwenye quality ndogo sana kumiliki dimba la kati,na kama Ole ameanza ujinga wake wa kumuacha Matic nje,basi we are in big trouble..Fred anaweza kucheza vizuri kushinda yeye Bigtime

Lindelof===What a softshit??...Watu wanasema Maguire ni mbovu kushinda Lindelof..serious?..huyu jamaa mlaini na mweupe sana..Hata Smalling hawezi kucheza vile..Tunahitaji CB

Rashford====Sioni ukuaji,nachoona kwake ni mchezaji ambaye kwa kipindi kirefu anakuwa out of form na naamini anakuwa anazidiwa hata na foward ya Engish Championship huko


Bruno+Pogba===Bado hamna kitu,,Yaani tangu Pogba ameanza kucheza na Bruno tumekuwa utopolo zaidi na haya mambo Ole
ni kama hayashughulikii

/////////

Tumetumia zaidi ya £800m toka Fergie aondoke zake lakini we aren't go no where..


Makocha pia wametuangusha sana,wamepewa wachezaji lakini pia wameshindwa kuwafanya wawe bora..leaving aside mambo ya kuletewa wrong choices
Serbia huko beki zipo kibao, tena bei rahisi.
 
Mechi ya kwanza maneno yamekuwa mengi hivi.
Sioni sababu ya kumlaum Ole wala wachezaji kwani ligi ndo kwanza imeanza.
Eti arsenal nao wanaisema man u, Arsenal acheni vituko.
Man u ndo tm ya dunia kwn hujui? Jana uwanja ulijaa utadhani man u vs Barcelona
 
Louis Van Gaal alisema

"Bayern ina CEO na watendaji ambao ni watu wa mpira, wanajua nini ni nini ila Manchester CEO alikua ni mwekezaji benki unaweza ona kwanini usajili hauchukuliwi serious"

Hapo Van Gaal alikua ni mhanga mwingine. Moyes alimsajili Fellaini ambaye miezi kadhaa mbele alikua anaenda kua free agent na market value ikiwa ni 23M ila bodi (Woodward) ikalipa 27M kumpata Fellaini.

Mourinho akaja na kutaka wachezaji 5. Kati ya hao 5 aliletewa Fred tu, kisha akasema anamtaka Maguire bodi (Woodward) akasema Maguire ni ghali sana kwa pesa iliyotajwa na kiwango chake hivyo waachane naye.

Otea ni beki gani amekuja kua ghali kuliko wote duniani....

So Mourinho akapigwa chini huku analalamika juu ya usajili. Kaja Ole, akauza striker akasema ana Rashford na Martial, hali ikawa mbaya wakafanya usajili kwa kupaniki wakamsajili Ighalo.

Familia ya Ighalo ilifanya sherehe baada ya kujua Ighalo kaenda Man U.

Kisha wakati wa usajili umefika timu inatafuta mabeki, wingers na viungo hakuna sehemu waliyosema wanahitaji striker ila kama kawaida mwisho wa yote lawama zitakuja kwa kocha na atatimuliwa aje mwingine.

System ya Man U ipo designed kufukuza makocha, tatizo la kweli ni kutokua na DOF nafasi ambayo Woodward aliifuta hiyo nafasi na kujikaimisha yeye. Na akasema hawana mpango wa kuajiri DOF.

Hii timu morali ipo chini, hili tatizo tulikumbwa nalo Arsenal chini ya Emery. Watu hawajielewi wanazomewa hawajiamini yaani vururu vururu naona Man U inapita same route na tayari hata mashabiki baadhi wanaamini Ole ana matatizo.

The system.
 
Back
Top Bottom