Kama kawaida leo mapema sana ntasogea karibu na TV kuona nini United watafanya.
Kwa misimu mingi mechi za ufunguzi huwa tunaanza vizuri sana haijalishi opponent tunayeanza naye.
Tukiamuaga ni mwendo wa 4 kwa kila anayekatiza mbele yetu, kuna msimu tulifungua msimu na Swansea akala 4 aliyefuata naye akala 4 na aliyefuata 4 hadi wakatuita wazee wa 4G. Msimu uliopita nao The Blauz wakachukua 4 zao safi na sajili zetu zote zikawa na mwanzo mzuri, Maguire & AWB walipata clean sheet na The Flash bwana Daniel James akamgaragaza Kepa Arizabalaga. 😂
Leo naiona United ikipata ushindi kuanzia goli 3 ikiwezekana tunapiga 4 palepale 'Theatre of Dreams' ama 'Stretford End' au 'Sir. Matt Busby Way' wenyewe wanapaita OLD TRAFFORD.
Tunaenda kuanza msimu tukiwa na nyota wetu muhimu kama Pogba, Fernandes. Nilishukuru sana Pogba ku-recover mapema maambukizi ya virusi vya Corona.
Mpaka sasa naamini Pogba ashajua mustakabali wake kisoka upo Manchester United naamini hii itampa morali kupambana zaidi uwanjani. Martial amekuwa na positive attitude sana tokea Bruno amekuja, naona kabisa msimu huu aki-shine zaidi.
Huu msimu iwe isiwe tutafanya vizuri sana tuna timu nzuri kupambana EPL tuna kiungo bora kabisa EPL.
Yote kwa yote hatutakiwi kuishia hapa tu, United wafanye tu maamuzi wamlete Sancho na Telles. Telles atatusaidia sana upande wa kushoto kupandisha mashambulizi hata ukabaji, jamaa physically yupo vizuri na ana shooting power kubwa; wenyewe wanasema msimu uliopita ligi ya Ureno yeye ni mmoja wa wachezaji bora pamoja na Bruno na jamaa ana fighting spirit ya kutosha ukimuunganisha na Bruno ni bonge la timu unajenga. Sancho kila mtu anajua uwezo wake akishika upande wa kulia itakuwa ni vilio kwa wapinzani kila wiki.
#GGMU