Soko siku hzi limebadilika na we dont hv to make a fool of anyone due to that.
Utd tulimuuza Ronaldo to madrid kwa approx £80mill kwa kipindi hicho ambapo kwa sasahivi ingekuwa juu zaidi..
Same na hapo naona price tag ya kipa ni £30mill( zaidi ya miaka mitano iliyopita) nafikiri kwa mwaka huu ni zaidi ya hiyo.
Kwa sasa tunaangalia thamani,ukiangalua thamani ya hicho kikosi kwa sasa ni zaidi ya mara mbili au tatu ya gharama za mwanzo. Ambapo huwez fananisha na gharama za Maguire.!!!
upo sahihi brother,
ila kuchafuka kwa soko la usajili barani ulaya na duniani kwa ujumla isiwe sababu au kichocheo kikuu kwa klabu husika kujiingiza kwenye biashara zisizo sahihi na zinazoweza kuepukika kwa kutafuta target mbadala.
klabu husika inapaswa iongozwe na sera imara zenye kuambatana na mipango madhubuti kwa kuanza na utumiaji wa wataalamu bora linapokuja suala la majadiliano ya mikataba na mauzo ya mchezaji lengwa, ufuatiliaji wa kiundani zaidi wa taarifa za mchezaji husika kwenye soko la usajili (ni vizuri zaidi ukafahamu mchezaji husika analengwa na timu gani nyenginezo na dau lao waliloweka na naamini si kosa kisheria), bila ya kusahau kuweka imani na wachezaji wanaotokea kwenye mfumo wa academy ili kujiepusha na hizo panic transfer za mara kwa mara.
baadhi ya maeneo hayo klabu ya bayern munich wameonyesha mafanikio (nimeangalia hapa wachezaji wengi wa bayern ukiachana na gharama ndogo za usajili pia mishahara yao inatembea kwenye wastani wa paundi elfu 80 hadi laki moja na thelathini, kwangu mimi hayo ni mafanikio makubwa sana kiuendeshaji wa klabu kwa njia ilio sahihi)
tatizo kubwa lililopo klabuni kwetu kwa sasa ni lile la kuingia kwenye harakati za kutafuta mchezaji mpya au kumshawishi mchezaji asaini kandarasi mpya tukiwa tayari tumeshaonyesha udhaifu wa uhitaji mkubwa wa mchezaji huyo, na hapo ndipo pande hasimu wanapoitumia fursa ya kutuingiza kwenye biashara zenye ugharama mkubwa kuanzia gharama za malipo pamoja na gharama za mishahara.
kwa mfano
juzi nimesoma taarifa isiyo rasmi inadai ya kwamba manchester united wanataka kumshawishi
dean henderson asaini mkataba mpya wenye thamani ya paundi laki moja kwa wiki, kama ningelikuwa nipo upande wa dean henderson basi ningelimshawishi atingishe kidogo biriti ndipo asaini kandarasi mpya (naamini upo uwezekano wa kuzidishiwa bonus), baadae akubali uamuzi wowote utakaofikiwa na klabu (either kutolewa tena kwa mkopo au kugombania namba).
kiupande wangu naamini paundi laki moja ni kiwango kikubwa sana cha mshahara kwa mchezaji ambaye hana uhakika wa kucheza kikosi cha kwanza na pia huu ukiwa ni msimu wake wa pili tokea acheze premier league tena kwa timu isiyokuwa na presha kubwa.
cha kustaajabisha klabu inakwenda kufanya majadiliano na upande wa henderson haliyakuwa tayari tumeshaonyesha udhaifu mkubwa wa uhitaji wa huduma yake kana kwamba hakuna target nyenginezo zenye uwezo wa kushika nafasi yake....
=====================================
mifano ipo mengi tu.......
ishu ya rashford kupewa mkataba wa kufuru (sina uhakika mkubwa ila mshahara wake unalingana na salah, lewandowski, aguero)
ishu ya degea kupewa mkataba wenye mshahara mkubwa (anafika paundi laki 3),
usajili wa harry maguire,
usajili wa wan bissaka (hapa zilikuwepo target nyingi mbadala),
usajili wa sancho (dortmund wameamua kutumia mbinu hii, wanajua tunafanana na barcelona kitabia)