Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Hapa sina haja ya kubishana

Ukweli wa Man Utd ulionekana baada ya Pogba, Martial, Greenwood kuingia

Usitake kuniambia majembe yenu mnayoyaaminia ni akina Tomori, Abraham
Mkuu usipoteze nguvu zako, achana nao hao lazima waongee, wao wenyewe hawaamini kama wameshinda jana, maana walishajiandaa kwa aibu kuu kama wangepoteza na jana.
 
Mkuu huoni vurugu hizi mnazoleta huku?? Jamaa yako mzee wa kujipiga BAN Ollachuga Oc kaweka kambi hapa.

Lakini tuongee Ukweli, unataka kuniambia mara tatu zote nilizokupiga nilisaidiwa?? Mimi nakubali jana mmetufunga kutokana na uzembe wa Kocha, Magwaya na De Gea, ila hamna kikosi cha kutufunga tukikamilika.

Anyways, hongereni mmeshinda isingekuwa vizuri mpoteze mara nne ndani ya msimu mmoja kwa timu moja.

Tukutane top 3, nani ataingia kule.
Kwaiyo jana mlikuwa tisa uwanjani

Angalia una Leicester na Westham ..awana cha kupoteza hao
 
Mkuu huoni vurugu hizi mnazoleta huku?? Jamaa yako mzee wa kujipiga BAN Ollachuga Oc kaweka kambi hapa.

Lakini tuongee Ukweli, unataka kuniambia mara tatu zote nilizokupiga nilisaidiwa?? Mimi nakubali jana mmetufunga kutokana na uzembe wa Kocha, Magwaya na De Gea, ila hamna kikosi cha kutufunga tukikamilika.

Anyways, hongereni mmeshinda isingekuwa vizuri mpoteze mara nne ndani ya msimu mmoja kwa timu moja.

Tukutane top 3, nani ataingia kule.
Olesendeka kashaomba tupoteze ili nyie muingie top 4, HONGERENI mna kocha wa maombi
 
EPL bingwa anachukua around £150m, ingawa hapishani sana na mshindi wa pili, na wakati mwingine namba mbili anaweza kuvuta zaidi ya bingwa, kuna vigezo.

UEFA hawachezi mbali na £80 - 90m.

Europa sina uhakika, mpaka kucheki kwenye mitandao.

FA ni around £3.5 mpaka 5m.

Hizo supercup pia sina uhakika lakini haziwezi kufika £1m.
Kumbe EPL anakula mpunga mrefu ivyo!! Kwanin sasa mkuu...me nnanvyojua UEFA ndo ina mpunga mrefu then epl afu FA ndo ije europa na mengineyoo..au!!!
 
Mkuu usipoteze nguvu zako, achana nao hao lazima waongee, wao wenyewe hawaamini kama wameshinda jana, maana walishajiandaa kwa aibu kuu kama wangepoteza na jana.
Tulishajiandaa kwa aibu kivip? Mpira una matokeo matatu ..kupigwa, kupiga au kutoa sare ...tatizo nyie mulikuwa na matokeo yenu mfukoni amuamin kilichotokea..sasa ivi kocha wenu anaomba tufungwe ili mpande top four, komaeni na Europa mbona simple tuu
 
tumeamua kujificha zaidi kwenye hoja ya uchovu uliosababishwa na mapumziko mafupi tulioyapata baada ya kucheza na crystal palace, labda ni kwa sababu ni jambo rahisi zaidi kuliongelea kuliko tactics, set up ya timu, team choice, aina ya wachezaji tulionao na style yetu ya kiuchezaji.
kwa kuweka kumbukumbu zetu kwa usahihi ni mason greenwood, pogba na martial ndio walianzia benchi kwenye mechi yetu ya jana kwa wachezaji wa kikosi cha kwanza baada ya corona.​

tukirudi nyuma Southampton kabla ya mechi yetu ndani ya siku sita walicheza na manchester city pamoja na everton na zote hizo ni team zinazocheza vizuri sana, soton hawana kikosi kipana kama sisi hivyo basi kwa kiasi kikubwa unakuta wachezaji wao wa kikosi cha kwanza wanacheza kwa dakika nyingi (lack of rotation) , kilichotokezea kwenye mechi ile wao walicheza vizuri zaidi kana kwamba wana kikosi kikubwa kutuzidi sisi.

hata kwa upande wa chelsea nao walikosa huduma ya pulisic na ngolo kante ambao wote ni wachezaji wa kikosi cha kwanza lakini bado walionekana kuwa vizuri zaidi kiuchezaji kuliko sisi,

kwa ufupi timu yetu inasumbuliwa na matatizo mawili makubwa sana ambayo hatupendi kuyazungumzia.
  • tunateseka mno tunapocheza na timu zinazojilinda (two blocks) hatupigi cross, hatuingii kwenye eneo la adui kiurahisi, rejea mechi yetu ya spurs kwa raundi ya pili na mechi zetu nyingi tulizocheza round ya kwanza ukiondoa ile ya chelsea (ile mechi walicheza kama kundi la walevi)
  • tunateseka zaidi na zaidi pindi tunapocheza na timu zinazo pressing: na hili tatizo limeendelea kuwa sugu zaidi na limeshakosa tiba na litaendelea kutusumbua, rejea mechi zetu na liverpool, manchester city, southampton (mechi zote mbili)
tofauti na manchester city (guardiola ni mwanadamu anayeishi na fikra zisizobadilika) , jana chelsea waliingia uwanjani huku wakiwa wameyafahamu fika matatizo yetu hayo mawili hivyo basi walihakikisha wanajilinda vizuri ( didn’t exploit their space ), pia wanatupa presha muda wote (kovacic ameendelea kuwa ni master wa kuzivunja timu pinzani) bila ya kusahau pressing in the final third wakiongozwa na giroud (muda mwingi alisababisha defence line yetu ivunjike)

ukicheza hivyo tu basi baadhi ya wachezaji wetu ukimuondoa nemanja matic wanakuwa clueless, panicky, lacking calmness under pressure na bahati mbaya zaidi hili tatizo hata benchi letu la ufundi nahisi wameshindwa kulifanyia kazi.

our pressing return imeendelea kuwa ni poor dhidi yao, Too often passes were misplaced, wachezaji wetu wanalose possession ovyo (wan bissaka anaongoza kulose possession and poor ball control) na hatimaye tunakosa mtego sahihi wa kuwawekea maadui (tunajificha kwenye failure counter attack)

kwa mfano
  1. mechi yetu ya mwanzo dhidi ya southampton tulilose possession mara 183 na mechi yetu ya marejeo dhidi ya hao southampton tulilose possession mara 141, ina maana benchi la ufundi walishindwa kuja na mbinu sahihi ya kuondokanwa na hilo tatizo
  2. United’s passing accuracy kipindi cha kwanza dhidi ya soton ilikuwa ni 81% lakini kipindi cha pili ilikuwa ni 71%
Swali la kujiuliza laiti kama tungelicheza na timu mfano wa cystal palace, aston villa, bournermouth na nyenginezo tungelicheza mpira ule wa jana kwa hoja ya uchovu?
sidhani
====================================
Sevilla wanatusalimia kwenye michuano ya Europa, kinyume chake tuombe watolewa na AS ROMA (tunalihitaji lile kombe)

marcelo bielsa amerudi (wengi wetu tunaikumbuka ile adhabu aliyotupatia akiwa atletico bilbao, waliokuwa hawajazaliwa kwenye soka kipindi hicho basi kamtafute iker munian, ander herrera wa siku ile na llorente).

klopp bado yupo

Southampton bado wapo na mjerumani

arteta msingi wake umeshaanza kukaza nadhani tumeiona pressing na rebuilding ya arsenal mechi za karibuni (goli la juzi waligusa mpira takribani mara 30)

tuendelee kujificha kwenye mfumo wa 3-4-3 au 3-5-2 huku tukiendelea kulipuuzia tatizo kubwa zaidi.
GGMU
===================
 
Mashabiki wa Man untd ndo wasumbufu sana wanaongoza kwa kuongea wa kishind
 
Kumbe EPL anakula mpunga mrefu ivyo!! Kwanin sasa mkuu...me nnanvyojua UEFA ndo ina mpunga mrefu then epl afu FA ndo ije europa na mengineyoo..au!!!

Hapana ligi inayoongoza duniani kwa soccer ni EPL.

UEFA inaweza kuonekana kama wanapata nyingi kwa sababu ya kulinganisha na idadi ya games timu inazocheza mpaka kuwa Bingwa.

Game 6 makundi, na game 6 mitoano (home and away) na game 1 final. Total ni 13 games.

Ukichukua £80m gawa kwa 13 unapata wastani wa £6m kwa kila game.

Wakati EPL mshindi wa mwaka jana alipata £149m kwa kucheza mechi 38, ambapo ni wastani wa £3.9 kwa game.

Ila ukifanya kwa jumla, hata mtu wa mwisho EPL anaweza kupata sawa na bingwa wa UEFA.

Ukipata muda pitia Thread ya Man City, ukurasa wa 492 kama unatumia web view yenye 20 posts per page.

Tuliwahi kulijadili hili, UEFA, La Liga na EPL.

Hapo kwenye UEFA isomeke €80 - 90m.
 
Kuna mambo yanashangaza sana, kikosi kilichokuwa na akina Phil Jones, Valencia, Ashly Young na Lingard mlitaka kichukue UEFA chini ya Mourinho, ila baada ya sajili kubwa zote , mnapigania kuingia nne bora huku wale pundits uchwara wakiwa wamefunga midomo. Unafiki ni kitu kibaya sana.
Msimu gani huo.
 
Kuna baadhi ya mashabiki wa Chelsea nimeona wanawaaminisha watu kuwa kombe la FA lina hela sana kuliko Man Utd kuingia UCL, kiukweli mashabiki wengi wa Chelsea huwa wana uelewa mdogo sana kuhusu football, ni kama wa Man City, Tottenham na mwakani Newcastle

Mwaka jana ma finalists, Watford na Man City walipata £1.8M kila mmoja.

Msimu wa mwaka jana Man City alipata £151M japo alikuwa mshindi na Liverpool alipata £152M. United alipata £143 na Arsenal alipata £142 japo Arsenal alimaliza ligi mbele ya United, hii inatokana TV deals. Hii ni kwenye ligi kuu.

Wakati ma finalists wa FA walilipwa £1.8M ma semi finalists walilipwa £ 0.9M

United asipokwenda UEFA Champions League msimu huu, atakatwa na Adidas £20M upward. Wakati huo huo United ataweza kupoteza potential deals kutokana na kutoingia UCL.

Kuna makala nilisoma United anaweza kupoteza up to £100M endapo hataingia UCL, kumbuka kila hatua UCL ina mpunga wake, tena mrefu.

Hapa sijaongelea kushindwa kusajili baadhi ya wachezaji nyota endapo United hataingia UCL.

Ni dhahiri shahiri OGS anatazama zaidi UCL qualifications kuliko FA, japo mashabiki tunataka vyote.
 
Hapa sina haja ya kubishana

Ukweli wa Man Utd ulionekana baada ya Pogba, Martial, Greenwood kuingia

Usitake kuniambia majembe yenu mnayoyaaminia ni akina Tomori, Abraham
Usijitoe ufahamu kwa Kanté na Pulisic hufahamu shughuli yao.
 
Mkuu huoni vurugu hizi mnazoleta huku?? Jamaa yako mzee wa kujipiga BAN Ollachuga Oc kaweka kambi hapa.

Lakini tuongee Ukweli, unataka kuniambia mara tatu zote nilizokupiga nilisaidiwa?? Mimi nakubali jana mmetufunga kutokana na uzembe wa Kocha, Magwaya na De Gea, ila hamna kikosi cha kutufunga tukikamilika.

Anyways, hongereni mmeshinda isingekuwa vizuri mpoteze mara nne ndani ya msimu mmoja kwa timu moja.

Tukutane top 3, nani ataingia kule.
Mla ndizi huwa hakumbuki ila muokota maganda lazima akumbuke. Nani asiyejua mara zote mmekua mkibebwa na maamuzi mabovu ya marefa? Lakini kwakua yashapita wacha tupotezee turudi kwenye mbio za top four. Naona keshokutwa utapanda mpaka nafasi ya 3 kwa muda baada ya kumfunga West Ham

Ahsante kwa pongezi.
 
Unaongelea majeruhi, mimi hao sijagusa hao kwa kuwa hawakuwa available, ni irrelevant kuongelea majeruhi

Kama una hesabu hadi majeruhi, hukawii kutaja mtakaosajili nao hawakuwepo
Usijitoe ufahamu kwa Kanté na Pulisic hufahamu shughuli yao.
 
Back
Top Bottom