Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Kule chelsea kuna mazombie tu, sasa mtu kama Ollachuga atachambua nin yule?? Labda kidogo cash money forever

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Matokeo ya mwezi December yanaweza kusababishwa na mambo mengi ikiwemo aina ya wapinzani tulipokutana nao mfano kati ya timu 3 tulizozifunga tukiwa tunatumia huo mfumo, mwezi huo ni Colchester (timu ya League 2) na AZ Akmar ya Uholanzi.

Pia timu yetu imekuwa haitabiriki kimatokeo inaweza kushinda mfululuzo au kupoteza mfulululizo bila kupata sababu za msingi (inconsistence)

Katika mechi 4 tulizoshinda hicho kipindi, mechi moja (dhidi ya Burnley), Scot hakuwepo, hatukucheza 4-3-3 na tulishinda 2-0

Formation ya 4-3-3 si siri ya ushindi au kupoteza, mfano kati ya Machi 10 hadi May 12, mwaka 2019 tulicheza mechi 10 na matokeo ya United yalikuwa ni W-2, D-2 na L-8. Katika hiki kipindi tulikutana wapinzani wakali mfano Barcelona mara 2, Wolves mara 2, Arsenal na Everton, hivyo Ukiangalia tu stats za kufungwa mfulululizo halafu uziusianishe na matokeo bado hutapata majibu sahihi

Let's say mfumo wa 4-3-3 ndio unatubeba (mfano hayo matokeo ya December uliyoyaainisha) , kwanini OGS asiutumie huu mfumo msimu huu, kwanini achague mfumo wa 4-2-3-1 unaompa matokeo hasi. Basi hii pia inadhihirisha kuwa OGS hajielewi.
Unazungumziaje december tulicheza 4-3-3 na tukadhinda 2+ mechi 4, baada ya majeruhi ya Mc tominay tukarudi na 2 man midfield?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu Rondo yupo ila amelikacha hili jukwaa kwa muda nahisi labda sababu ya mwenendo wa timu ulivyo...

Ila mkuu umenichekesha kuhusu chelsea mbona kule kuna mtaalamu mbobezi wa masuala ya soka kaka mkubwa Ollachuga Oc mpe credit zake walau kidogo basi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwishoni mwa february Herrera anapata injury ya Hip anamiss mechi 6 na man utd inaanza ku struggle, mfumo ukabadilika, mfano hii mechi ya Arsenal tulicheza 4-4-2

Refer mechi za psg, barca na mechi nyengine za kipindi kile tulikuwa tunacheza na 2 man forward mainly lukaku na rash.

Unasema ole ni mjinga kwanini asichezeshe 4-3-3 unatakiwa ufahamu midfield ili icheze 4-3-3 inabidi uwe na midfield watatu mmoja specialist wa kulia, mwengine kati na mwengine kushoto, kwetu kulia ni wawili tu Herrera na Mc tominay, na msimu huu kwa majeruhi ya matic, dogo mc tominay anacheza kama holding wa kati, hivyo hatuna kabisa mid ya kulia. Na tetesi nyingi za sisi kununua midfield zilikuwa zinasema kabisa right side midfield


Na hata midfield tuliemsajili bruno fernandez anacheza kama mid wa kulia kwenye 3 man midfield japo pia anaweza cheza kama holding na attacking centre.
 
Kwahiyo mechi zote hizo 12 nilizozitolea mfano OGS alikuwa hatumii mfumo wa 4-3-3 ndio maana United alikuwa kwenye form ya kushuka daraja?

Unataka kusema mfumo wa 4-3-3 ni bora kuliko mifumo yote ikiwemo wa 4-4-2, 3-5-2, 4-2-3-1? Mifumo yote ni mizuri with the right players, depending on the opponent you face. Mfumo sio kila kitu. Kuna mechi nyingi tu tumetumia mfumo wa 4-3-3 na tukapigwa


Kwa kocha mzuri, Fred anaweza kucheza vizuri tu mid ya kulia kama mbadala wa Herrera

Umesema OGS alicheza December mfumo wa 4-3-3 kwa kuwa alikuwa na wachezaji wa kufanya hivyo, nakumbuka kwenye pre season na wakati tunaanza msimu kila mtu alikuwa fiti na Ole aliutumia mfumo wa 4-2-3-1. Unataka kuniambia hawa waliocheza December hawakuwepo mwanzoni mwa msimu wakati tunapiga Chelsea 4-0 kwa mfumu wake wa katikati kuwa na 2-3? OGS hajui anachofanya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa tunaofahamu mashindano tunayoshiriki kwa msimu tuliongea kabla msimu haujaanza kikosi chetu ni kidogo na tukipata majeruhi ya key players 3 tu timu itapotea,huwezi kuondoa 5 players kwenye timu bila replacement na hizi option za kusajili free agent na wachezaji wa mkopo ambazo OGS amehangaika kuzifanya January zilipaswa kufanyika tangu summer na alikuwa anasema yuko comfortable na wachezaji aliokuwa nao

That was another big mistake aliyofanya OGS baadae ikamlazimu kuwachezesha wachezaji wakiwa injury (Pogba,Rashford,McTominay) waliumia kocha akawachezesha kabla hawajawa fit baadae wakapata injury za muda mrefu.

Majeruhi ni kitu hakiepukukiki ndio maana timu zinakuwa na wachezaji wengi Liverpool wamepata majeruhi ya Alisson,Gomez,Matip,Lovren,Fabinho,OX,Keita .City Aguero,Sane,Laporte,Cancelo,Mendy
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pre season tayari Herrera ameondoka, na kama ulivyosema ndio kocha anatumia mfumo kutokana na wachezaji alionao.

Pia nikukumbushe fred hajawahi kuwa na wenzake wote akiwa fit msimu huu, alienda kuoa pre season na mpaka ana regain fitness na kurudi kikosi cha kwanza tayari pogba na matic ni majeruhi, akakaa 2 man midfield na Mc tominay.

Na tunatumia sana 4-4-2 ama 3-5-2 kwenye mechi kubwa tunazoshinda kwa counter hivyo hii pia ni mifumo yetu tunayofanya nayo vizuri. 4-3-3 inatusaidia kutoboa low block timu zinazopaki basi.

Kwanini 4-2-3-1 inakataa na 4-3-3 ikubali? Jibu ni rahisi hatuna no 10 ya maana kwenye 2-3-1 wakati 3-3 yenyewe haitumii no 10 bali creativity inatoka kwa hizi midfield za pembeni ndio maana pogba alikuwa ni crucial sana kwenye huu mfumo.

Na toka pre season nilikuwa naliongelea hili leo angekuwepo Dybala wala tusingeona haya mapungufu kwenye 4-2-3-1 na angekuja bruno mapema 4-3-3 ingeendelea. Na mifdfield zetu zote 5 zikiwa fit sitashangaa tukiswitch 4-4-2 diamond
 
Herrera aliuzwa wakati alikuwa key player kwenye 4-3-3. Na hakuletwa mchezaji wa kumreplace Ander. Hiyo ni akili au matope?

Hata mashabiki waliona upungufu wa timu wakati tunaanza msimu. Kikosi kilikuwa chembamba sana. Kwanini kocha alikuwa comfortable wakati ule? Na wengi wakasema, ikiwa tukapata majeruhi tutatafutana humu. Na kweli tukapata majeruhi.

Wachezaji kupunguza morali baada ya kocha kupewa mkataba ni kosa la nani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unazungumziaje december tulicheza 4-3-3 na tukadhinda 2+ mechi 4, baada ya majeruhi ya Mc tominay tukarudi na 2 man midfield?
Kwahiyo tulitakiwa tuwe na options hata tatu kwenye kils namba. Ambapo kabla dirisha kubwa kabla halikufungwa, tulitakiwa tuwe na silaha za kutosha incase matatizo yakatokea. Si ndio?

Manake haiingii akilini timu kubwa na tajiri kama Man Utd inaanza msimu bila striker na midfield mmoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Brother, Wolves, Arsenal na Everton sio timu kali kama tunavuojaribu kujifikirisha.

Ni kwamba standards za United zimeshuka sana. Almost kila kocha alikuwa anaifunga timu ndogo kama Arsenal. Why now?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Thats my concern.

Kocha alikuwa very comfortable kuuza wachezaji. Why?

Tena ni key players.

Alitegemea kina Tahit Chong au Greenwood ndo wampe matokeo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hili linajulikana na sio tu kusajili bali structure nzima kuanzia sehemu za mazoezi, viwanja vya mazoezi, team ya madaktari, etc vinatakiwa viangaliwe sababu rate ya majeruhi toka moyes atimue staff wote wa fergie ni kubwa sana. Hakuna kocha post fergie ambae hajasumbuliwa na majeruhi 10+
 
Okay. Tuachane na majeruhi.

Manake hata timu kubwa wanakumbana nalo.

Je, mbadala wa key player kupata majeruhi upo wapi?

Kocha amejipangaje kwa hilo.?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…