kwa mara ya kwanza nimeangalia highlight za bundesliga msimu huu kwa sababu ya huyo haaland.....
pale borussia amezungukwa na thorgan hazard, fundi jadon sancho na marco reus.
kwa hii style ya uchezaji wa haaland kama atakuja manchester united hii ya nyakati hizi tungelikuja kumtukana bure ed woodward, ole na haaland mwenyewe.
utofauti mkubwa uliopo kati ya greenwood na haaland ni kwamba mmoja wao kila timu anayokwenda anakutana na wachezaji wanaojua kumhudumia mshambuliaji.
niliwahi kuandika humu ndani ya kwamba mason greenwood amezungukwa na wachezaji vilaza ndio maana tunaogopa kumuingiza moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza...
greenwood kiufungaji anamzidi hata yule dogo wa barcelona mwenye thamani ya paundi millioni 40...
utofauti wao unabaki pale pale kwenye kupewa huduma stahiki (mwenzake amezungukwa na messi, griezmann, suarez, de jong n.k)
man utd hii inahitaji mshambuliaji anayejitafutia huduma mwenyewe mfano wa kylian mbappe, sergio aguero, carlos tevez, wayne rooney, luis suarez na karim benzema.
greenwood anajua kujiweka kwenye maeneo ya hatari kuliko mshambuliaji yeyote tuliyenaye.
imagine huduma zile anazozipata yesu wa manchester city aliyezungukwa na debruyne, sterling, mahrez, silva brother zimgeukie mason greenwood.
licha ya kuwa na uhaba wa washambuliaji ila kuikosa huduma ya haaland hakujanichukiza.