Kwa sehemu kubwa mpira wetu tunacheza counter attacking, na timu inafanikiwa tu kwa counter attacking kwa timu inayokuja kwako kukushambulia, maana wanaacha nafasi kubwa kutoka kwenye 18 yenu kwenda golini kwa mpinzani
Timu ndogo huwa hazishambulii sana, na nyingi zinapocheza na timu kubwa (kama United) huwa zinacheza pia counter attack. Kiufupi hizi timu huwa zinatumia style ya low block. Style ya low block hairuhusu counter attack (Uwanja unakuwa mdogo kwa wanariadha kama akina DJ, Martial na Rashy)
Ili uweze kuvunja defense ya timu ndogo inayopaki (inayocheza low block) unapaswa kuwa na watu watundu kama akina Hazard, Silva, Messi n.k. Au uwe na wapiga pasi zenye macho kama De Bruyne, Scholes, Pirlo n.k. Na hawa watu kwa sasa hatuna.
Mata katika kiwango chake angeweza kutusaidia, Pogba katika ubora wake anaweza kufanya hiyo kazi. Lakini kwa sasa wote hawawezi, mmoja umri umemtupa mkono, mwingine hana consistence.