timu inaweza kuwa na mwalimu hodari kimbinu na mikakati lakini akakosa wachezaji sahihi lakini pia timu inaweza kuwa na wachezaji sahihi lakini ikakosa mwalimu mwenye mipango mizuri ya kutafuta ushindi.
ni nadra sana kuikuta timu kubwa ikikumbana na matatizo yote hayo mawili kwa wakati mmoja, bahati mbaya sana kwa muda huu man utd tunasumbuliwa na matatizo hayo mawili kwa wakati mmoja.
- kipindi cha kwanza kocha anakuja na mikakati mizuri sana ya kupambana na liverpool na hatimaye mipango inafanya kazi kwa dakika 45, tulifanikiwa kumdhibiti kiunganishi kikuu roberto firmino, bila ya kumsahau origi, robertson na mdogo wake arnold alexander, na wakati huo huo liverpool walikuwa na mwanadamu sanamu uwanjani asiyekuwa na athari yoyote na hapa namkusudia captain henderson,
- ushawadhibiti wachezaji watano kwa mkupuo mmoja lakini cha kusikitisha tukashindwa kuitumia nafasi hiyo adhimu kwa kukosa kwetu wachezaji sahihi. ndani ya dakika 45 tunafanya shambulizi moja tu la hatari zaidi na ndilo lililotupa goli na baada ya hapo kama kawaida yetu ni mwendo wa kulose posession kwa wachezaji wetu utafikiri timu yetu haifanyi mazoezi kila siku, sijui yule andreas perreira alifanya maamuzi mangapi ya ovyo akiwa eneo la hatari la adui.
- kipindi cha pili timu inarudi uwanjani ikiwa na mawazo ya kujilinda, ok ni sawa unalinda kwa muda wote huku midfields yako ikiundwa na claudio makele, mikel obi, michael ballak na michael essien tena dhidi ya barcelona ya xavi au gaucho. Kibaya zaidi tulikuwa tunalinda chini zaidi (karibu ya eneo letu la kujidai na kuzidi kuikaribisha presha).
- unamruhusu trent alexander na robertson wafanye wanachokihitaji kama wanavyofanya kila siku,unategemea kitu gani ukiachana na neno bahati ipo upande wetu, wakati kipindi cha kwanza ulikwisha wadhibiti na hawakuweza kuleta athari yoyote ile golini kwako?
- wakati huo huo liverpool walishaingiza wachezaji wawili muhimu wenye uwezo wa kutembea na mipira kwa uhakika tofauti na wachezaji wa kwetu sisi. kivyovyote kitakachofuata ni adhabu tu na si chengine au uokolewe na neno bahati ilikuwa upande wetu.
tumepata suluhu kwa udhaifu wa timu yetu kwa ujumla na si kwa ubora wa liverpool kwa mechi ya jana.
liverpool walipocheza na barcelona waliipata nafasi kama ile tulioipata sisi jana ya kuwa pungufu kabla hatujabadilisha mfumo na kilichotokezea kila mtu anakifahamu.