kuna video fulani niliiangalia zamani kidogo inamuhusu jose mourinho tokea akiwa ndie kocha wa manutd msimu wake wa pili, ilikuwa ni siku mbili baada ya kufungwa na sevilla kupitia michuano ya champions league, jose mourinho alitumia takribani dakika 12 kuizungumzia hali halisi iliopo ndani ya klabu ya manchester united kwa takribani miaka 8 pamoja na timu nyenginezo.
jose alisema ya kwamba ni sahihi kulaumiwa kwa sababu ya matokeo mabovu dhidi ya sevilla lakini kufungwa kwetu na timu ya sevilla si jambo la ajabu kwa sasa kwa sababu man utd imeshakosa
football heritage, hivyo basi inahitajika mipango madhubuti yenye kuambatana na muda wa kutosha kuijenga upya manchester united ili irudi tena katika ubora wake.
mara ya mwisho kwa man utd kucheza fainali ya champions league ilikuwa ni msimu wa 2010/2011 chini ya sir alex ferguson, kiupande wangu nathubutu kusema ndio fainali iliokuwa nyepesi zaidi kumtambua bingwa kabla ya mechi kuchezwa kwa kulinganisha ubora wa vikosi vya timu mbili hizo, msimu huo mchezaji bora wa ligi pamoja na klabu yetu alikuwa ni nemanja vidic.
Licha ya kubeba ubingwa wa ligi kuu msimu huo kwa tofauti ya alama 9 dhidi ya chelsea na manchester city lakini kiwango chetu cha jumla kilikuwa ni cha kawaida sana na ndio maana haikuwa ajabu kutoa suluhu mechi 11 japokuwa tulifanikiwa kukusanya alama 80 pungufu ya alama 2 tulizokusanya msimu wa 2017/2018, ukimuangalia jirani yetu imewachukua miaka miwili tu kuweza kujenga timu ambayo iliweza kujiingiza kwenye kinyang'anyiro cha kuchukua ubingwa (man city walishaonyesha dalili za kuwa tishio ila bahati mbaya mashetani wekundu wakaendelea kulala).,
mwaka mmoja baadae (msimu wa 2011/2012) man united tulipangwa kundi moja na timu nyepesi za
basel, benfica, galati kutoka romania kwenye michuano ya UEFA, cha ajabu makamo bingwa alitolewa hatua ya makundi. Hatukuishia hapo tu pia tulitolewa kwenye hatua ya mtoano wa league ya europe dhidi ya
athletic bilbao ya marcelo bilesa kwa magoli 5-2, msimu huo athletic bilbao walishika
nafasi ya 10 kwenye ligi ya hispania. Miaka minne baada ya city kununuliwa na matajiri wa kiarabu hatimaye msimu huo walifanikiwa kubeba ubingwa kwa tofauti ya magoli dhidi ya man utd.
msimu wa 2012/2013 man utd tunafanikiwa kubeba ubingwa kwa utofauti wa alama 11 dhidi ya man city huku ukiwa ni msimu wa tano tokea man city inunuliwe na matajiri wa kiarabu kama nitakuwa nipo sahihi, ndani ya miaka mitano man city walizidi kujenga emperor yao na kuwa dominance kwenye top 3 ya ligi kuu, hatukuishia hapo tu pia msimu huo tulitolewa hatua ya
16 bora kwenye michuano ya ligi ya mabingwa dhidi ya real madrid ya jose mourinho. hatimaye sir alex akastaafu kufundisha soka.
ina maana miaka mitatu ya mwisho ya sir alex ferguson ilionyesha muelekeo wa timu kupanda juu (2010/2011), kushuka chini zaidi (2011/2012) baadae ikapanda kidogo (2012/2013),
huu ndio usajili alioufanya sir alex ferguson miaka mitano ya mwisho.
chris smalling = amefeli kuwa mrithi wa
ferdinand tokea nyakati za fergie mwenyewe mpaka leo
phil jones = amefeli kuwa mrithi wa
vidic tokea nyakati za fergie mwenyewe mpaka leo
alexander buttner = amefeli kuwa mrithi wa patrice evra tokea nyakati za fergie mwenyewe na leo hatujui yuko wapi
ashley young = alicheza vizuri mechi za mwanzo ikiwemo ile ya ushindi wa magoli 8 dhidi ya arsenal, baada ya hapo alipata majeruhi na hakuonyesha tena uwezo wake tuliouzoea tokea akiwa wattford na aston villa iliokuwa ikifundishwa na martin oneill, kutoka kuwa winga machachari hadi kuwa mlinzi wa pembeni
chicharito = alicheza vizuri sana lakini baadae akapoteza nafasi walipokuja walimu wengineo ambao hawakuvutiwa na uchezaji wake
robin van persie = ulikuwa ni usajili wa muda kutokana na umri wake kuwa mkubwa.
shinji kagawa = alishindwa kufikia matarajio ya klabu ndani ya uwanja.
bebe = sijui yuko wapi huyu bwege.
antonio valencia: alisajiliwa kwa dhumuni la kuziba nafasi ya ronaldo yule aliyeondoka manchester akiweka rekodi ya kufunga magoli 40 kwa msimu mmoja, kituko usajili huu haukuwahi kutupa hata magoli 5 kwa msimu mmoja, miaka yake 10 amefunga magoli 17 tu, Baadae aligeuzwa kuwa mlinzi wa pembeni.
gabriel obertan = sijui hata aliishia wapi huyu dogo.
michael owen = mfugaji farasi mwenziwe aliamua kumsitiri
david degea = huu ndio usajili pekee wa fergie unaoendelea kutupa faida ile tulioitegemea tokea kusajiliwa kwake.
kwa mtazamo wangu hawa ndio wachezaji ambao walishaanza kuonyesha dalili za kuchoka kisoka miaka mitatu ya mwisho ya utawala wa sir alex ferguson na bahati mbaya kama nilivyosema hapo juu walishindwa kupatikana warithi sahihi wa nafasi zao tokea fergie akiwa madarakani.
ji sung park
rio ferdinand
nemanja vidic
ryan giggs
darren fletcher
patrice evra
paul scholes: (alistaafu akarudishwa kana kwamba timu haina pesa)
darren gibson
tom cleverley
anderson: (kiwango chake ilikuwa ni sawa na maji kupwa na maji kujaa)
luis nani: hakuwahi kucheza vizuri mechi 10 mfululizo.
anguko letu lilianzia hapa