ngoja nichomoe nyuki waliolala muda huu:
kwa uoni wangu dhaifu miaka minne ya mwanzoni tokea akabidhiwe timu sidhani kama itakuwa ni sahihi kumhukumu sir alex kwa kushindwa kufanya vizuri kwa sababu aliikuta timu ikiwa ovyo sana na ilihitaji muda kuingiza idea na sera mpya za uendeshaji wa klabu ndani na nje ya uwanja ikiwemo kurudisha nidhamu bora ya kiuchezaji , tukumbeke ya kuwa hakuikuta united ikiwa kwenye ubora kama ilivyo nyakati hizi kifedha na hata kimipango endelevu.
kwangu mimi nautizama zaidi udhaifu wa fergie kutoka mwaka 1999 alipobeba treble hadi mwaka 2008 ambapo ni takribani miaka 10 ambayo alikaa bila ya kubeba ubingwa wa ulaya na wakati huo huo ndani ya miaka 10 hiyo kama nitakuwa nipo sahihi amebeba ubingwa wa ligi takribani mara sita, inawezekana zipo sababu nyingi zilizopelekea kukaa tena muda mrefu bila ya kubeba ubingwa wa uefa ikiwemo ushindani mkubwa kutoka kwa wapinzani kama vile ac milan, munich, madrid, na wababe wengineo.
je ligi kuu ya uingereza nayo ilikuwa ni dhaifu sana ndio maana fergie alikuwa anabeba ubingwa mara kwa mara kabla ya ujio wa matajiri wengineo mfano wa roman na mansour?
je inawezekana ujio wa matajiri mfano wa abramovich ulichochea kumtoa ferguson usingizini na hatimaye akatengeneza tena timu ya ushindani kama ya mwaka 1999 iliofanya vizuri kwa miaka mitatu mfululizo ndani na nje ya uingereza?
kwa timu aliyoijenga fergie nyakati zile baada ya kutoka kushinda makombe matatu (kizazi cha giggs,nevile brother, cole, yorke, beckham, solskjaer, keane, scholes, butt, stam) na nguvu aliyojaaliwa kuwa nayo kimatumizi ambayo aliijenga kwa nguvu na jasho lake mwenyewe (rejea usajili wa rio, veron, nistelrooy, rooney, berbatov, nani, anderson) hakupaswa kukaa tena miaka 10 ndipo abebe tena ubingwa wa ulaya, angalau ingelikuwa kila baada ya miaka 5 amebeba ubingwa basi ningelizidi kumpa heshima ya kuwa manager bora wa karne.
kwangu mimi namtizama sir alex kama ni mwalimu ambaye ndoto yake kubwa aliyokuwa anaipigania ni kuona anavunja kwanza utawala wa liverpool kimafanikio kwenye ligi kuu ya uingereza na si kuvunja mafanikio ya liverpool na timu nyenginezo kwenye ligi ya mabingwa.
mbona guardiola ana champions league mbili kwa miaka 10 ya ufundishaji wake soka?
mbona mourinho ana champions league mbili kwa miaka 15 ya ufundishaji wake soka?
mbona ancelotti ana champions league tatu kwa miaka yake 24 ya ufundishaji soka?
mbona zidane ana champions league tatu kwa miaka yake minne ya ufundishaji soka
maswali na majibu
tumuache sir alex ferguson apumzike.