lakini chief unaweza kuwa na umri mkubwa lakini ukawa na maarifa madogo hivyo hivyo unaweza kuwa na umri mdogo lakini ukawa na maarifa makubwa sana.
rooney amekuja man utd mwaka 2004 akiwa na miaka 19
ronaldo amekuja man utd mwaka 2003 akiwa na miaka 18
mpaka mwaka 2007/08 wote kwa pamoja walikuwa na umri wa miaka 22 hadi 24, hivyo basi inawezekana walikuwa bado na umri mdogo lakini walikuwa tayari wana uzoefu mkubwa sana wa kucheza mashindano makubwa na hili limechangiwa zaidi na viwango vyao vya kiuchezaji.
rooney, tevez, ronaldo, nani, anderson, vidic, evra walikuwa ni vijana kiumri lakini walikuwa ni wazee tukiangalia uwezo wao wa kucheza soka.
rashford ni kijana kiumri lakini pia ni kijana kiuwezo wake wa soka, umri huu wa rashford nyakati zile michael owen ameshaanza kutishia ulimwengu wa soka
kabla ya umri huu wa rashford, wayne rooney anawafunga arsenal akiwa na miaka 16 na miaka miwili baadae anasajiliwa kwa paundi millioni 24 na bwana fergie.
bila ya kusahau umri huu wa rashford bwana xavi hernandez hakuwa mchezaji anayetajika sana ukilinganisha na umri wake wa miaka 28.
Age is a case of mind over matter. If you don't mind, it don't matter