simchukii daniel james kwa asili yake alipozaliwa bali ni kwa kiwango chake cha wastani alichonacho kinachongezwa udambwi udambwi na media za kiingereza wakiongozwa na legend ryan giggs, binadamu tunatofautiana sana kiuelewa inawezekana wenzangu mumenizidi mno hivyo basi pengine mtazamo wangu juu ya daniel james ni dhaifu.
kwa mujibu wa situation ilivyo ndani ya manchester united uwezekano wa kusajili winga mpya haupo hivyo basi tunakwenda kumbebesha majukumu mazito huyu bwana mdogo haliyakuwa huko anakotoka hakuwa fundi kama neymar yule wa santos au frank ribery yule wa olympique marseille na uthibitisho wa hilo ni hizo takwimu zake na video zake kwa wale ambao hatujawahi kumuona dakika 90 zinatuonyesha ni mchezaji wa aina gani kwa kutumia macho yetu dhaifu.
kwangu mimi namuona daniel james ni species ile ile iliotuzalishia wright phillips, theo walcott na oxlade chamberlain (wazee wa harakati nyingi kama pimbi). klabu ilipaswa kwanza itafute winga ambaye ameshauthibitishia ulimwengu kiubora ndipo baadae tumtumie daniel james kama ni nyongeza kwenye kikosi kama ilivyo manchester city wanavyomtumia phil foden au liverpool wanavyomtumia shaqiri.
kama daniel james ataniaibisha mbele ya jamii kwa kuonyesha kiwango bora basi tutakuwa tumeramba dume na nitakuja kuomba radhi humu ndani kama nilivyofanya kwa ole gunnar solskjaer, si hivyo tu atakuwa ni mchezaji wa pili kuniaibisha baada ya zoran tosic.
lakini ikiwa kinyume chake tutakuwa tumekula hasara kwa sababu itatulazimu tena kuendelea kumtumia juan mata na jesse lingard upande wa kulia ambao wamekwisha feli kwa muda mrefu na jambo hili sitaki kuliona likitokezea tena.
alichokosea bwana ole ni kumweka daniel james kama ni kipaombele chake cha kwanza kwenye usajili ndio maana si ajabu kumuona bwana ed woodward amemkimbilia huyo kijana kwa sababu ni rahisi kumpata.
ni rahisi sana kulipa paundi millioni 50 kwa mchezaji baadae ukalipa tena paundi millioni 15 kwa mchezaji anayecheza nafasi ile ile.
ni rahisi sana kulipa paundi millioni 15 kwa mchezaji lakini ni vigumu sana kulipa tena paundi millioni 50 kwa mchezaji mwengine anayecheza nafasi ile ile.
View attachment 1148508
hivi ni nani anayemdanganya ole gunnar solskjaer kama atapewa muda mrefu wa kujenga timu kwa kutumia wachezaji ambao ni underdog kama alivyo yeye na CV yake ya ukocha?
ni nani aliyemwaminisha bwana ole ya kwamba wachezaji wa kiingereza ndio pekee wenye haki miliki ya kuzipigania timu (wazalendo)?
Manchester United 'preparing bid for Longstaff'
United are reportedly preparing a bid for the Newcastle midfielder Sean Longstaff.
However, Sky Sports say Newcastle will demand a fee in excess of £50million for the 21-year-old.
Longstaff’s current deal at St James’ Park runs until 2022.