Kwenye hoja ya kwanza nipo na wewe 100%, ni ujinga kulazimisha mchezaji abaki na wakati yeye hataki kubaki, japo timu nyingine ni ving'ang'anizi mfano Klop aliwahi kulazimisha Lewandosk abaki pale Dortmund, Bayern wakaja wakamchukua bure
Kwenye suala la pili, ni kwamba ni kweli potential na proven players wamefeli pale United. Swali ni kwamba ni bora usajili mtu kwa £50mil+ halafu a flop au usajili kwa £12mil ili hata aki flop iwe hasara ya kawaida na atafutwe mchezaji mwingine?
Na point yangu ya msingi, United hawana utamaduni wa Galacticos, na tulivyo adopt huo utamaduni mambo ndio yakawa mabaya zaidi, kwanini tusiende back to our roots?
Guys, kilichotokea MUFC sio Galactico signings, binafsi sijaona wachezaji walokuja MUFC ndani ya miaka sita tangu aondoke Ferguson ambao unaweza kusema kuwa ni wachezaji moto. wachezaji waliokuja ni wazuri ila sio wakupewa sifa ya ki galactico.
Mkuu, kwa mimi (Nazungumzia mfano ningekuwa manager) wote wa 50 na 12 million, si expect waje kuflop. Yaani mmoja akiflop, regardless of their price tag ujue basi kuna tatizo, ama hakustahiki kununuliwa kwa pesa izo na alikuwa over priced ama nimeshindwa kumdevelop, ama nimebuma mimi kumnunua mchezaji sie. Ata Fergie makosa haya yalimkuta.
Tatizo letu tumekuwa tunanunua wachezaji for the sake of signings.
Sipingi kuleta vijana kuja MUFC, lakini tunampa mkataba Young na kumuacha herrera, miaka nenda miaka rudi tumeona Jones na smalling hawatufai ila bado wamebaki Club!.
Halafu inawezekana hamukunielewa, mnafikiria kama mimi nataka tununue ma stars tu, mimi nataka wachezaji wenye experience na wanaojua kazi zao. Mtizameni Pep alivojenga timu, mpe milioni miliono 100 atakuletea wachezaji wawili ambao in a very short time wanakuwa tishio.