huwezi kukimbilia kujaza wachezaji klabuni haliyakuwa waliopo hwajapata sehemu ya kujisitiri, kufanya hivyo ni kuongeza kiwango cha gharama za matumizi ya mishahara.
huwezi kukimbilia kumnunua wan bissaka au mounir haliyakuwa hufahamu mustakabali wa matteo darmian, kama ataondoka itakuwa ni faida kubwa sana kwa sababu gharama zake za huduma zitahamia kwa mchezaji mwengine.
inter milan wanahitaji kwanza kumuondoa mauro icardi ndipo watafute mbadala wake kati ya lukaku au edin dzeko, ndio maana wapo tayari kufanya swap deal mbele ya man utd au AS Roma.
juventus wanavutiwa na huduma ya pogba lakini wapo tayari kutupa dyabala na mchezaji mwengine kwa mujibu wa taarifa.
real madrid kama kawaida yao wanafanya biashara ya ununuzi kwanza then ndio watafanya biashara ya kuuza,ujio wa hazard, jovic, mendy na wengineo utaondoka na bale, james rodriguez, navas na wenngineo.
barcelona wameganda kwenye usajili wa antoine griezmann, unamleta griezman na de ligt lakini umtiti, coutinho, dembele, rakitik, malcom, vermaelen bado wamegoma kuondoka na release clause ni kubwa.
ina maana gharama za mishahara zitaongezeka klabuni kwao kama wote watakusanyika kwa pamoja.
ukija kwetu ni nani anayemuhitaji sanchez?