Hakuna uhusuiano wowote wa wa position ya CEO na kujua mpira.
Hakuna uhusiano wowote wa CEO na vipaji vya wachezaji kupanda au kushuka.
Hakuna uhusiano wowote wa CEO na Benchi la ufundi.
CEO wa Liverpool ni
Peter Moore hakuwahi Kucheza mpira, kuujua mpira, wala hakuwahi kujishughulisha na Chochote kinachohusu mpira kabla ya kuteuliwa CEO na Liverpool mwaka 2017.
Ni mfanya biashara tu na si vyenginevyo! Kutokujua kwake mpira hakuhusiani na Vipaji vya Kina Mane, Salah, VVD and co.
Kwa historia Yake fupi unaweza hata ukapitia hapa →
https://en.m.wikipedia.org/wiki/Peter_Moore_(businessman)
Na hawa CEO wa timu nyingi huteuliwa/Huajiriwa kwa taaluma za Kibiashara na si kwa kujua mpira kwani Mpira ni biashara, na cheo cha CEO ni cha kibiashara kusimamia mapato ya timu.
Narudia tena kuboronga/Kuporoka Vipaji kwa Wachezaji ni Poor coaching and Management kwa kocha.
Ni jambo la ajabu kumlaumu Woodward na kusema hajui mpira kwa Kushuka kiwango Martial au Pogba!! Ed anahusikaje na vipaji vya wachezaji? Is he Coach? Psychologist?
Huwezi kusema Ed hajui mpira wakati yeye ni Mfanya biashara! Hata kama ataondoshwa leo hii, basi mwengine atakayepewa nafasi si Cantons wala Dwight Yorke bali ni Mfanya biashara mwengine mwenye uwezo wa kumanage Business in best way kuingiza more profits, na si kuajiri mjuzi wa Mpira.
Sawala la kutoa hela za kunulia Wachezaje ni Chairman ndiye anayehusika kwa 100% na si only Ed kama watu wanavyojiaminisha.
Hivi Chairman/Mmiliki atenge Budget ya £300m kwa ajili ya Wachezaji then Ed anaoubavu wa kusema hatozitoa? Aende nazo wapi?
Sasa Kama Chairman/Mmiliki katoa £150m kwa ajili ya usajili, Ed afanyeje unadhani? Atatumia alichopewa.
Lazima watu wafahamu na kueka mipaka majukumu ya CEO na Technical Staffs.