Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Kwahy alishinikizwa? Dadavua
Hakushinikizwa ila alisoma mambo yanavyoendeshwa akaamua aondoke asuharibu heshima yake.

Maana baada ya SAF kuondoka hata Moyes alisuasua sana kwenye issue ya usajili.

Na juzi kati alisema hakumuhitaji Fellaini ila aliletewa na Ed kilazima.
 
Zlatan 35 !,sijui kama mwalimu unategemea nini kwa mchezaji mzee wa kiwango hiki zaidi ya kuwazibia nafasi makinda.

Sanchez 29 kama kuna mchezaji majanga sijaona kama huyu,kwanza kaja kuharibu salary structure na sijaona anachokifanya zaidi ya kuanguka angua uwanjani na kulalamika kwa waamuzi.

Matic 29 alicheza mwaka 1 baada ya hapo hakuna kitu akiwa uwanjani ni kama team inacheza na wachezaji 10,yuko very slow hapa sasa ndio utajua umri ni suala muhimu sana.Kwa lugha rahisi Matic umri umemkamata kisawa sawa hana mchango wa maana katika team bora McTominay mara mia mbili.
Huyo Zlatani (35) unayemponda, ndio striker aliyefunga Magoli mengi pale United kuliko striker yoyote kwa msimu tangu aondoke Van Persie (29). Na hapo aliumia kabla ya msimu haujaisha

Embu nitajie ni wachezaji wangapi kwenye ligi ya Uingereza waliofunga magoli zaidi ya 29

Zlatan ameondoka, amewaachia vijana nafasi akina Lukaku, Rashford, Martial, wamefunga Magoli mangapi kwa msimu huu, au uliopita. Hakuna cha maana. Angalau hata Lukaku anajitutumua.

Ukiondoa Matic, Sanchez niambie hao wengine wenye umri unaoupendekeza wewe, wameifanyia nini United? Niambie aliyekuwa na 27 alifanya nini, niambie Bailly aliyekuwa na 22 amefanya nini? Vipi kuhusu Pogba (24), Dalot na wengine?

Kwa kigezo chako cha umri, mazingira yakiruhusu usajili Messi (32), Ronaldo (33), Griezeman (28), Aguero n.k utakataa kuwasajili na badala yake utamchukua Odoi, Rashford eti kwa sababu wao ni wadogo? Magoli watakayofunga hao jamaa "wazee" ndani ya misimu 3, itawachukuwa hawa "watoto" pengine carrier yao yote
 
Arsenal wako mbele kumhitaji Zaha.. kuna tetesi wako tayari kutoa wachezaji wawili + pesa ili wamchukue.
Hakim Ziyech pia amesema anapenda kucheza Arsenal na yuko tayari kuondoka pale ajax.
Ziyech aliyasema hayo mwaka 2017, leo ni mwaka 2019

Mick aliwahi kusema anapenda Arsenal, akaanzia United
 
Zlatan alicheza vizuri msimu mmoja tu,msimu uliofuta alichemsha vibaya sana,again umri hasa EPL si suala la kubeza.Ukitazama League ya Italy aina mchezo unaweza kuwa accomodate wachezaji wazee lakini si EPL.Naamini Man inatakiwa kutazama mipango ya muda mrefu kuanzia Mwl na Wachezaji naamini katika usajili wa makinda ndio suluhu ya matatizo yetu ya muda mrefu.

itazame Ajax tuliyokutana nayo fainali ilijikita zaidi katika makinda sisi tulikimbilia fainal product matokeo yake ndio haya tunashindwa kuingia top 4.Uwekezaji wa kina Pogba.......unatuumiza sana kuanzia fedha zilizotumika na baya zaidi tabia zake mbovu za kujiangalia yeye mwenyewe kuliko team ni mwendelezo wa mifano mibaya kwa wachezaji chipukizi.
Zlatan msimu wa pili ni kama hakucheza (sidhani kama alianza hata mechi 5)

Kwa hiyo huwezi kum judge kupitia msimu wa 2 ambapo ndio alikuwa ametoka kwenye majeruhi mabaya sana
 
Usajili wa Jose karibu wote haujatick sema katika hali ambayo waliikuta team ilikuwa lazima ichukue muda sana kuibadilisha.
Van Gaal aliwanunua.
1 Sergio Romero
2 Matteo Darmian
4 Daley Blind
5 Angel Dimaria
6 Memphis Depay
7Morgan shenerndalin
8 Luke shaw
9 Ander Herera
10 Radamel Falcao
11 Anthony Martial
Kati ya hao wote ni wachezaji wanne tu walionyesha angalau usajili umelipa.

Moyes aliwasajili hawa.
1King Fella
2 Mata
Angalau walionekana kuwa na maana hasa Mata msimu wa Van gaal

Mourinho aliwasajili hawa.
1 zlatan
2 mikhtarian
4 Lindelof
5 Bailey
6 Fred
7Pogba
8 Lee grant
9 Dalot
Katika list yote hii hakuna waliokaa vizuri kwenye squad hata chini ya Mourinho mwenyewe
Sijui hapa umetumia kigezo gani

Ila kama usajili wa Van Gaal unasema angalau wachezaji 4 walionesha makeke, usajili wa Jose unamuachaje Pogba, Matic msimu wa kwanza, Zlatan pia
 
Ziyech aliyasema hayo mwaka 2017, leo ni mwaka 2019
Mick aliwahi kusema anapenda Arsenal, akaanzia United
Sawa.. Arsenal wako bize na Zaha lakini ikishindikana wanaweza kumvuta Ziyech sisi tumezubaa mno.
 
Utamuuza Rashford + Lingard hukosi £100M unaongeza £60M unamleta Mbappe.
Man United hawezi kosa hela ya kumleta Mbape, maana kitita pekee atakachokabidhiwa ni kati ya £200m na £250m

Ameambiwa mchezaji akiuzwa hiyo hela itaongezewa kwenye kitita cha manunuzi

Swali ni kwamba, je hao Mbape wapo tayari kuja OT?
 
Sasa unadhani Kocha gani atakayeuza wachezaji hao wote 3?

Mimi huwa si intervene mawazo yenu lakini ukweli ni Kwamba hao madogo (Rash, Ling na Mart) ni natural talented players ambao wanahitaji good coaching tu!
Bali kwasasa wanaonekana ni useless kwasababu system ya uchezaji wa timu hijawa suitable kwa wao.

Na vile vile timu nzima imekosa Morali jambo ambalo wenye vipaji na uwezo wanacheza kama Mrisho Ngassa.

Kiukweli hata kama Top Management (Ed na genge lake) lina matatizo kocha anatakiwa angolee kama kama Kila kitu kipo sawa na hakuna lolote linaloendelea.

Unay Emery anapewa Limited Budget ambayo haitozidi £100m lakini anaongea kwenye Media na Wachezaji kama Everything is alright.
Sasa hivyo ndiyo Kocha anavyotakiwa awe ili apandishe Moral ya Wachezaji.

Sasa Ole hana talent of Wisdom ya kupandisha psychology na Moral ya Wachezaji kwenye kupambana.

Hapo patafutwe kocha ambaye atacheza na Psychology za wachezaji ili afichue vipaji vilivyojificha vya kina Rash, Ling na Mart.
So far Ole anatupa mashaka, lakini ni mapema sana kum judge kwamba hana uwezo, hana wisdom na blaa blaa nyingine

Tunampa benefit of doupt kwanza
 
Usajili wa pogba na Sanchez ulichangiwa zaidi na ambition ya Management kwa sababu ya kibiashara na sio target ya kocha kwa 100% ....wakat mwingine ni ngumu kumbishia boss wako, japo mambo yakiharibika ww ndo unakuwa responsible....
Ni kama ya Perez kumng'ang'ania James Rdriguez huku Anceloti hana mpango nae, mwisho wa siku mambo yakaenda vibaya Anceloti akafukuzwa kazi
Upo sahihi

Unaambiwa Sanchez usajili wake ambao ulifanyika majira ya baridi (msimu usio maarufu kwenye usajili kama summer) uliongelewa zaidi kwenye social media kuliko usajili wa Neyamar wa £199m kwenda PSG

Hivi ndio VITU ambavyo Ed akikaa na ma investors anaviongelea, STUPID
 
Back
Top Bottom