Antonio ni Dreams come True,alikuwa anaipenda Man United sana,Inasemekana kipindi anapata taarifa ya kutakiwa na SAF (Sir Alex Ferguson) alisitisha Matibabu na kuondoka katika kambi ya Wigani.
Antonio namfananisha na Wimbo wa Daz baba ft Ngwair (R.I.P) -WIFE.
Daz baba Moja ya mashairi yake
"Long-time Namzia huyu sholi/
Ila sjawahi naye hata kupiga story/
Ila niliamini yeye ndiye atakaye nifaa/
Siku moja moja nimekaa maskini nashangaa/
Kupokea yake barua yeye anadai Mimi ndio namchengua/
Hata jibu sikujua nikamwambia mama moyo wangu wote chukua"
Antonio hakuamini kilichotokea kutua Old Trafford.
Hahahaha kuhusu lugha umenikumbusha kuhusu Tevez, alishindwa kabisa kujifunza lugha ya Malikia
Antonio huko nyuma akiwa Wigan na wakati anahamia United, niliijua hiyo story ya kushindwa kui master lugha ya kiingereza, lakini alivyokaa United na baadaye akakabidhiwa kitambaa cha unahodha sijui kama tatizo la lugha liliendelea (logic yangu, ni mchezaji anapewaje ukapteni kama hana uwezo/anawasiliana kwa tabu na wachezaji wenzake?)
Valencia aliwahi kusema alivyokuwa anacheza huko kwao Ecuador, kuna siku alikuwa home na Familia ya kwao wanaangaalia mechi moja pale Nou Camp, akawaambia ipo siku nitacheza hapo, basi Familia yake wakiwemo wazazi wake wakamcheka sana. Anakwambia miaka kadhaa mbele (alivyokuwa United, akaichezea United dhidi ya Barca pale Nou Camp). Hii story ilinifundisha jambo kubwa sana kwenye maisha yangu
Antonio ni fighter sana, lakini umri umemtupa mkono. Ngoja tusubiri mbadala wake kwenye usajili dirishi hili.
Kuhusu lugha ya Malikia mpaka nyakati hizi Antonio bado si mzuri sana ukilinganisha na Juan Mata na Herrera waliomukuta England.
Kuhusu Ucaptain wa Antonio na lugha ya mawasiliano kama kiongozi,
Kwa mabadiliko ya kisoka Nyakati hizi Ucaptain kama umeshushwa vigezo hapa ndiposa tunapata kuwaona akina Messi/Ronaldo ambao kwangu mimi sioni sifa kutoka kwao katika uongozi katika Timu,
UCaptain imekuwa kama aidha ukongwe wa Mchezaji ndani ya klabu Au Umaarufu/Nembo ya klabu/Bembelezo la Mchezaji kubaki ndani ya klabu kwa hiyo kwa namna hiyo mchezaji anaweza kupewa UCaptain hata kama anauwezo mdogo sana(Ububu pia) wa vigezo vya Ucaptain....Tofauti na captain ni Mtu muhamasishaji,Mwenye kukemea uzembe,kuunganisha Timu na kuongoza timu katika nyakati zote(Mfano great Captains ,Patrick Viera,Roy Keane).
Carlos Tevez hahaha Jamaa alikuwa fighter kuna jamaa yangu mmoja alikuwa anamkubali sana alivyoondoka Old Trafford Jamaa aliumia sana na kuwekwa benchi UEFA champions final 2009 Barc vs Man United. Huyu jamaa naye hakujisumbua na lugha ya Malikia mpaka anondoka Epl inasemekana hafahamu lugha.
Ramires Mdigo wa Brazil aliyekuwa akipendwa Chelsea huyu pia pamoja na kukaaa muda London haifahamu lugha.
Saizi Kun Aguero inasemekana lugha ndio haipandi kabisa,kipindi cha nyuma mchezaji mwenzake Zabaleta ndiye alikuwa mkalimani wake.
SIR ALEX aliwahi kusema lugha ni moja ya changamoto kubwa sana haswa kwa Wachezaji wa kigeni.
Klopp huwa anawisisitiza wachezaji wake watie bidii kujifunza lugha ya Malikia ili irahisishe kazi ya ukufunzi,
Watu wa Lugha ya Malikia wanapata fursa kwa kufunza lugha wachezaji wenye nia na uhitaji.