Lukub
JF-Expert Member
- Feb 5, 2012
- 3,790
- 4,284
Hongera mkuu kutubu ni indicator ya ushujaa na wala sio udhaifuDECEMBER 19 / 2018
tusione aibu kutubu dhambi zetu
ewe bwana Mungu si ungelitupa japo kauwezo kidogo wa kujua maisha yetu ya mbeleni sisi binadamu
nilisifia sana ujio wa ole gunnar solskjaer kwa sababu nilikuwa na imani ya kwamba wachezaji walishamchoka jose mourinho ndio maana tulikuwa tunafanya vibaya na nilifikia hatua ya kuandika maneno yafuatayo
kama solkskjaer atafanya vizuri basi klabu impe mkataba wa muda mrefu na isihangaike na makocha wengineo kama zilivyofanya klabu nyenginezo kama barcelona na madrid. hizi si nyakati za kupima ubora wa kocha kwa kutumia hoja ya uzoefu bali mafanikio yake ndio yatazamwe kwa jicho la mwewe, unajua kama kenny daglish ilimshinda liverpool lakini jurgen klopp anaelekea kufanikiwa.
lakini pia nilisisistiza maneno yafutayo ambayo bado yanaendelea kuwa sahihi.faida kubwa ya ujio wa ole gunnar solskjaer ni kwamba hatatokea yeyote anayejiita legend ambaye atathubutu kumkejeli mungu mwenye sura ya kitoto, hutomsikia paul scholes, giggs, neville brother,ferdinand na wengineo wakinyanyua mdomo wao kama mambo yatakwenda vibaya, labda awe mzungu asiyependa unafiki kama roy keane.
kama solakjaer atafanya vibaya hao legend wote watamgeuzia kibao ed woodward na watasema ya kwamba yeye ndio tatizo kwa kushindwa kutofautisha soka na biashara, pia watamshambulia paul pogba na wachezaji wengineo ambao watashutumiwa hawaithamini nembo ya klabu bali wanathamini maslahi yao.
mwisho nikamalizia
kumsubiria ole gunnar solakjaer afanye vibaya ni sawa sawa na kumsubiria kylian mbappe afikishe miaka 20 ya kuzaliwa au kumsubiria romelu lukaku afunge goli mita 30 kama wayne rooney.
radika naomba unisamehe brother, uliona mbali sana pale uliposema tutabadilisha makocha wangapi ikiwa mahitaji ya makocha hayatimiziwi?