Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Nadhani tunahitaji kujenga timu kama ambavyo tunawaona ajax hapo, sosha tumemkabidhi gari mbovu, tusimlaumu inapomisi na kuzima njiani, sisi wenyewe tulipotea katika uendeshaji wa timu yetu na uwezekaji wetu mbovu,
Leo hii lionel messi analipwa zaidi pale barca na hispania nzima, anatuweka goli tatu jumla hadi sasa, wakati sisi mchezaji tunayemlipa hela nyingi zaidi united na uingereza yote hata kuingia kikosini tu ni kwa kubahatisha, na yuko mkeka, pengine ata asicheze,
Tuione tofauti yetu, barca ni timu, hawaungi ungi wachezaji, ajax ni timu, hawaungi ungi wachezaji, juve ni timu, na wanaongeza watu wa kuwapa matokeo zaidi, tunacheza na timu ambazo kwenye kikosi chetu labda mchezaji mmoja tu anaweza ingia kwenye vikosi hivi vya wapinzani wetu,
Hata aje nani man u saivi, hawezi kufanya maajabu, tuwe na subra tuu,
Tujenge timu, ubingwa tusahau kwanza, tuweke pembeni...tukubali sisi ni washindani tuu kwa sasa, sio washindi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom