fedha ya kufanya matumizi ya wachezaji kuanzia 6 hadi 8 sidhani kama ipo kwa msimu mmoja kama tutaamua kutafuta wachezaji wa bei ghali, na kama haipo hata msimu ujao mwendo utaendelea kuwa ni huu wa kucheza vizuri mechi tano then tunacheza ovyo mechi 5 (inconsistent).
kama target zetu ni wachezaji wanne ina maana antony martial, jesse lingard, nemanja matic, smalling, ashley young, rashford, shaw wataendelea kuwa wachezaji wetu wa kikosi cha kwanza msimu ujao.
mwanzoni ilikuwa ni man city peke yake lakini kwa sasa liverpool nao pia wanatuzidi kiubora kama utawalinganisha mchezaji mmoja mmoja. ukimuondoa lindeloff na paul pogba ambaye nayeye kiwango chake hakina tofauti na majira ya msichana (menstrual) sidhani kama tuna mchezaji mwengine mwenye uwezo wa kucheza kikosi cha kwanza pale liverpool.
allison vs degea ( kwa sasa namchagua allison)
arnold vs young ( hata mwendawazimu atamchagua arnold)
robertson vs shaw ( takwimu zinambeba robertson)
virgil vs smalling (virgil mchezaji bora wa mwaka)
matip vs lindeloff (victor yupo vizuri)
gini vs matic (gini yupo vizuri)
fabinho vs herrera ( kwa sasa fabinho)
lallana vs pogba (pogba)
salah vs rashford ( salah ameshuka kiwango lakini bado ni bora)
firmino vs lingard ( hata malaika watamchagua firmino)
mane vs martial ( mhhhhhhhh mane is the best baada ya aguero kwa msimu huu)