Watu wanaotaka tusajili Full Back wana hoja ya msingi
Ashley Young msimu ujao anafikisha miaka miaka 34 na kushinda kombe na full back wa miaka 34 ambaye alibadilishwa kutoka kuwa winger ni jambo gumu sana
Valencia, Darmian msimu ujao hatutakuwa nao tena pale United, hilo lipo wazi
Hii itatufanya kubaki na Shaw, Dalot na Young (ambaye umri si rafiki kwake/kwetu) kwa nafasi za full backs
Nikitazama Academy sioni full back wa ku take over kwani madogo tulionao umri bado hauwaruhusu kucheza katika level ya juu. Kuna dogo anaitwa Ethan Laird ((RB) na Brandon William (LB)
Nikichungulia waliopo loan, namuona TFM na Borthwick Jackson, are they good enough for tilltle surge? I don't think so. Pia yupo Tuanzebe ambaye anaweza cheza full back, lakini kwa asili ni CD.
Option nyingine ni kuchezesha wachezaji out of position. Bailly anaweza kucheza FB, Ice Man anaweza kucheza full back, pia Jones na Smalling wanaweza kucheza full back. Tukumbuke tunampango wa kununua CD, hivyo hawa jamaa wanaweza kupisha mgeni (hope it is Koulibally). Lakini je tunaweza kuchukua kombe kwa kuchezesha wachezaji out of position, SIDHANI.
Kwahiyo tunarudi pale pale kwamba ni kweli tunahitaji FB.
Lakini je tunahitaji full back kama tunavyohitaji Central Defender, Midfielder na Winger mpika mabao? HAPANA. Je Ed/Glazers wapo tayari kutoa mpunga wa kusajili wachezaji 4 (world class players)? SIDHANI. Nadhani, nasisitiza nadhani utatoka mpunga wa kusajili wachezaji 3.
Hivyo kama Ed atatoa mpunga wa wachechaji 3 (jambo ambalo nawaza ndio litatokea), tunapaswa kutazama options ya madogo wa academy ama waliopo loan ili kuwa na back up ya full backs next season. Lakini mpunga wa wachezaji 4 ukitolewa naona ni jambo la lazima kununua full back
Wan Bissaka au nani? Ni ukweli usiopingika kua dogo ni mzuri sana, lakini pia tuna dogo mwingine ambaye pia ni mzuri, anaitwa Dalot. Hivyo katika kununua beki ninaona ni vyema tukinunua more experienced full back, mfano Thomas Meunier wa PSG (shabiki kindaki ndaki wa United) au Sidibe wa Monaco. Hiyo ni mifano tu, tunaweza kupata mabeki wengine. Hawa mabeki wazoefu watamfanyia Dalot mentoring akiendelea kujifunza.
Huo ni mtazamo wangu masela msijenge chuki (Utani tu)
Sent using
Jamii Forums mobile app