Naona wengi wetu tumeridhika kuondoka kwa Herrera, japo mimi ninaona tatizo
Ni ukweli huko ulimwenguni kuna upgrade ya Ander lakini si wengi kama tunavyodhani
Kupata mbadala wa Ander tunahitaji sio chini ya £50 million, hivyo kama Glazers walitaka kumpa Ole £200 million kwa ajili ya kuimarisha kikosi, watapaswa kutoa £250 million jambo ambalo siamini kama Glazers wapo tayari.
Glazers watamwambia Ole, mtumie zaidi Tominay, mtumie zaidi Fred, mtumie zaidi Perreira na ikibidi angalia academy lakini sidhani kama kuna hela watatoa. Tukumbuke kuwa kabla ya suala la Herrera tayari tulikuwa tunahitaji kusajili midfielder mmoja, sasa itakuwa wawili.
Watu wanasema tutampata Rabiot bure, jambo ambalo sio kweli kiivyo maana kuna signing on fee £10 million. Isitoshe ninampenda Rabiot kama mchezaji, lakini character yake na mama yake ambaye ni agent wake ni tatizo. Ku deal naye ni mtihani sana, yupo kama Pogba tu. Isitoshe sio sisi tu tunaomtaka Rabiot, kwa hiyo kuna competition na kwa kuwa ni free agent lazima ata demand mshahara mkubwa tu.
Kama tulikuwa tunataka sana kufanya surgery ya kikosi, katika midfield Matic ndio alikuwa wa kwanza kuondoka kabla ya Herrera. Matic ana mwaka 1 wa kucheza kwa kiwango kinachohitajika pale United, na Herrera alikuwa ana misimu zaidi ya 2 kucheza kwa kiwango cha juu
Kibiashara Ed na Glazers sijui wanawaza nini? Kwanini basi wasikubali kumpa mshahara wa £200k kwa wiki anayodai halafu akitokea mteja auzwe hata kwa £25million? Mbona tulifanya hivi kwa Fellaini? Jambo pekee ninaloona hapa United wali abuse upendo aliokuwa nao Herrera kwa United, wakidhani "kuku akiwa wako, hamna haja ya kutumia manati ili kumpata"
Let's wait and see
Sent using
Jamii Forums mobile app