Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Mkuu usiongelee kijuu juu ongea kwa big picture nita round up pengine comments ya mwisho.

1. Mnasema wametumia 600m ila ni double counting, mchezaji ananunuliwa na kuuzwa na hela inayopatikana ananunuliwa mwengine, investment ni ile iliobaki, mikhi hayupo, di maria hayupo, depay hayupo, falcao hayupo, blind hayupo etc wote hao ni zaidi ya 100.

2. Tumetumia hela nyingi kipindi cha lvg si kuimprove kikosi bali kureplace wachezaji ambao tumewacha waondoke either kizembe ama kutokuwa na mipango thabiti, nikakupa mfano beki watatu world class wa kutegemea wameondoka pamoja, evra, vidic na Rio, si jambo la.mchezo same kwa idara nyengine.

3. Usajili wa Woodward mara nyingi upo motivated na potential ya mchezaji kuja kufanya vizuri kibiashara na sio kuziba pengo uwanjani mfano nimekupa wing ya kulia, LVG miaka anataka Robben au mchezaji mwenye kasi hakuletewa, same kwa mou alisema anataka winga/winga wa kulia kumtupia cross Lukaku, Ameshindwa hata kumleta perisic. Hadi leo kwa Ole dalot alicheza winga ya kulia unaona jinsi Lukaku anavyokuwa hatari, Na ole nae anataka wings ya kulia Vile vile. At same time tumesajili martial, di maria, depay, sanchez etc wote wapo comfortable kucheza kushoto. Mkuu huoni tatizo?.

Kifupi mkuu timu yetu haina identity hatujulikani tunataka nini hebu angalia hii list ya makocha 4
-Moyes
-LVG
-Mou
-Ole

Hakuna hata mmoja anaefanana na mwenzake na kila kocha anahitaji kuanza upya alipoishia mwenzake, huyu mid table mentality, huyu mwengine anataka pass fupi.fupi na speed, huyu ana defend sana, mwengine anashambulia sana na mpira wa kasi wa counter etc, identity yetu sisi ni ipi? Angalia timu kama Barcelona, wana identity yao na usajili wao unaendana na hio identity, hata wakichukua makocha ni nadra kuona wanafeli.

Timu kubwa zote ulaya na baadhi ndogo zina strong foundation ya watu wanaojua soccer angalia Bayern, Ajax, Barcelona, Man city, juve, etc huko utawakuta kina Van de sir, Olivier, Nedved, tixi etc wote wachezaji wakali wa zamani wanaojua mpira nini na wameprove kuwa waendesha timu wazuri. Sisi tunapoach watu kwenye mabenki na ukitoa Kocha uongozi mzima ni clueless wa mpira.
 
Ni kweli mkuu matokeo ya uwanjani in long term ndio yatakayo determine uwezo wetu wa kifedha, ila the way man u ilivyojengwa hata kabla haijaanza kupata mafanikio ilianza kuingiza hela ndefu. man UTd ni brand kama Cocacola ama Nike hata timu ilivyoshika nafasi ya 6 bila kombe ilizipita madrid na Barca kimapato.

Na ukumbuke mkuu Glazer ni mfanyabiashara, akiitumia man u kulipa madeni yake yote na kuchota mpunga wa kutosha siku akiona mambo yanaanza kuwa mabaya financially anenda kutuuza arabuni ama china na yeye anasepa. Hakuna mkataba wowote kwamba lazima awe hapa miaka yote, hivyo hakuna ulazima kwake kujali hayo ya baadae.
 


Labda tulikuwa hatujaelewana vizuri mi sio kwamba nasema hii club haina matatizo hapana, matatizo ypo na nakubali unachosema kuhusu hilo swala la kukosa Identity na kumuajiri Woodward afanye kazi za Dof wakti wote tunafahamu Jamaa ni Banker, ila kwa mada ulioanza nayo ile ya Glazers hawatoi pesa hapo ndo nilipokuwa napinga! Hilo swala la Double Counting nalo si kubaliani nalo coz hata kwa Net Spent bado tupo juu zaidi Mancity ndani ya hii misimu mitano iliyopita.

Ni kweli hii Club toka Ferguson na David Gill wameondoka imekosa identity na hii nikutoka na nakushindwa kujiaandaa mapema kabla babu kustaafu, kweli hili walipaswa kuliona kina Glazer na hata babu ilitakiwa awashauri kuleta watu wa maana ili kwenda na wakati, ukiangalia kikosi alichokiacha babu wachezaji wengi walikuwa ni wazee na wameshashuka sana viwango hvyo ilipaswa Dof aletwe mapema ili kuwa replace wakina Vidic na top players lakin hawakufanya hvyo,sababu hata babu alikuwa hapendi kufanya kazi na Dof na ilikuwa sio tamaduni za UTD kuwa na Dof.

Shida hapa ni kwamba Kina Glazer mpira hawajui wanahitaji washauriwe na ndo maana Fergie mpka leo yupo pale kwa kazi hyo sema babu nae bado alikuwa na mambo ya kizamani sana mfano Hazard alikuwa anauzwa Million 32 na Lille babu akakataa kumsajili kwasababu tu alikuwa hataki kudeal na Agent wake aliekuwa anataka chajuu na wakati ilikuwa wazi kabsa Hazard atakuwa Top player na kwa kipindi kile tulikuwa tunahitaji winger na sio kwamba hela ilikuwa haipo sema tu alikuwa hawapendi ma agent kama alivyogombana na Mino Raiola,matokeo yake Chelsea wakamchukua and the rest is history.

So mkuu usione tu eti kwasababu mchezaji flani hajaja ukajua ni makosa ya Woodward hapana sometimes hata wachezaji na Club zao wenyewe wanazingua, mfano Robben,Muller,Bale,Thiago na Fabregas wote walikataa kuja wao wenyewe sio swala la hela tu,Hyo Persic Inter walitaka kuleta Uhuni walijua tna shinda na winger hvyo wakapandisha bei yake mara 3 wakati mchezaji mwenyew umri umeshaenda baadae wakasema eti tubadilishane na Martial kitu ambacho Club ilikataa na mimi niliona ni sawa, coz Persic muda wake umeshapita na si mzuri kiasi hicho.

Woodward kuletwa pale UTD Glazers hawakukosea kwa mtizamo wangu coz mpka sahv Club inaingiza mapato mengi sana ukilinganisha na Mwanzo kwa sababu yake, yeye ndo kaleta masponsor wengi wanaotoa mpunga mrefu pale ila tu kazi yake ilitakiwa awe CEO tu na Kazi ya Dof wangempatia mtu mwenye uzoefu wa Soka,kama Dof angekuwepo toka mwanzo hizo hela walizotoa Glazers mpka sasa zingetosha kbsa kuwa na kikosi cha maana na Coach anaeenda na Misingi ya Club.
 
Haya Mou kaondoka, mahitaji ya defender yapo au hayapo?

Kumbuka hao defender watano ni

Rojo-spana mkononi
Jones-
Smalling
Bailly
Lindelof

Sent using simu mbovu
Tunapaswa kuwaoffload kwanza hao ndiyo tuseme kuwa tunahitaji defender tatizo la Mourinho alishindwa kuwatumia hata aliowasajili yeye mwenyewe kisha akahitaji pesa tena.

Bila shaka matumizi kama hayo hata kama wewe ni Woodward usingeapprove.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeongea point defenders watano timu inafungwa na Newcastle na Brighton haifungi magoli bado tuendelee kutoa pesa.?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Woodward ana mwajiri Mourinho ambaye tunamfahamu ni kocha anayetaka ready made players ,anamuongezea mkataba na anagoma kumpa fedha za usajili then anamfukuza na kumlipa £20ma

Sent using Jamii Forums mobile app


Kwani Mbona Chelsea walimwajiri Mourinho na Kumfukuza na Kumwajili tena na Kumfukuza hukushangaa?? au Mbna Hukushangaa Wenger Kukaa miaka yote hyo Arsenal bila Kufanya lolote la maana?? Au Madrid Kumwacha Zidane aondoke alafu wanarudi kumsajili tena??Au Bayern Kumruhusu Heynckes Kuondoka alafu kumrudisha tena?? Hivi vitu ni kawaida kwenye mpira mzee na Makosa hutokea Kwenye Club zote tu sio UTD peke yake!
 
Haya Mou kaondoka, mahitaji ya defender yapo au hayapo?

Kumbuka hao defender watano ni

Rojo-spana mkononi
Jones-
Smalling
Bailly
Lindelof

Sent using simu mbovu

Kwani hao defenders si ndo hao hao waliocheza mechi 12 unbeaten na OLE na tukaanza kufurahi ama hivi vichapo viwili vya Wolves na Arsenal ndo vimekubadilisha mtizamo mkuu? Ukweli ni kwamba Mou alikuwa anataka kutuaminisha kwamba hawajamaa hamna kitu kabsa wakti kwa Kocha mwingine unaona sio kweli alichokuwa anadai!
 
Akiendelea kuhoji mitashangaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mario Balotelli was wearing a t-shirt with Marcus Rashford on it under his Marseille shirt & intended to unveil it if he scored vs PSG



SOMA HILO BANGO HAPO CHINI
 
Umeongea point defenders watano timu inafungwa na Newcastle na Brighton haifungi magoli bado tuendelee kutoa pesa.?


Sent using Jamii Forums mobile app
Pep ametumia paundi mil 200 kununua mabeki ,timu zilizomfunga Man City ni Newcastle,Crystal Palace,Leicester lakini owner still wanaendelea kumsapoti sababu wanajua project wanahitaji nini
 
Lakini record zinambeba Ronaldo ambaye chances ya kuscore kwa free kick ni kubwa kuliko kwa Messi

Sent using Jamii Forums mobile app

Hapana hii sio kweli mkuu Ronaldo ana goli nyingi zaidi za freeckick kuliko Messi sababu ame attempt kupiga freekick mara nyingi zaidi (kwenye mashinda yote) lakini ukiangalia huwa anakosa kwa rate kubwa kuliko Messi ..check namba zinavyosema kwa La liga

The Argentine has now scored 28 free-kicks from 330 attempts in LaLiga, with a conversion rate of 8.5%

Ronaldo struck 19 free-kicks for Real Madrid in Spain's top flight, a tally he reached in 310 attempts, which is a conversion rate of 6.1%.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…