I think you read what Arsene Wenger said about the match.
 
Wakati wadau wa GOONERS wakishikwa shati(2-2) na watoto wa malkia birmingham..Wale wazee wa vingunguti leo wamefanya kile kilichotarajiwa kwenye tawi lao la Saint James Park...
Rooney...Ronaldo(2)....Saha....Raha Tupu ndani Machinjo
.....MAN U..5 Newcastle 1
Tumebakiza point3 tuwe juu ya msimamo wa ligi na kwenda kunyakua kombe..mambo yanaanza kwenda kombo dakika hizi za lala salama wa wadau wa emirates...Adui yako muombe njaa na mikosi tu:)
 
Manuuuuuuuuu yaaani weeh acha tu....

Pamoja na kuwapongeza vijana wetu kwa kazi nzuri, lakini hatuna budi kuziba hilo pengo la pointi. Hawa vijana washika bunduki watachonga sana iwapo watatuacha nyuma.
Uzi huo huo Man U
 
Ili uwe na furaha inapasa tupendelee Man U..


Ila sasa hivi acha tuongee bwana maana tukifungwa huwa hatupati raha kwa mashabiki pinza na jirani.

Ila kiukweli hawa wana wanatisha jamani kama njaa maana ndani ya wiki moja yaani ukihesabu jumamosi iliyopita mpk jumamosi ya jana tumeshinda goli 11

Arsenal vs Man Utd - FA 0-4
Lyon vs Man Utd - UEFA 1-1
Newcastle vs Man Utd Premier 1-5

Sasa nahisi kunakuanza kupata majeraha maana wengine sidhani kama wanaweza kukubali Maafa.

Mungu ibariki Man Utd
Mungu ibariki Jamboforum
 
Ila sasa hivi acha tuongee bwana maana tukifungwa huwa hatupati raha kwa mashabiki pinza na jirani.

Ila kiukweli hawa wana wanatisha jamani kama njaa maana ndani ya wiki moja yaani ukihesabu jumamosi iliyopita mpk jumamosi ya jana tumeshinda goli 11

Arsenal vs Man Utd - FA 0-4
Lyon vs Man Utd - UEFA 1-1
Newcastle vs Man Utd Premier 1-5

Sasa nahisi kunakuanza kupata majeraha maana wengine sidhani kama wanaweza kukubali Maafa.

Mungu ibariki Man Utd
Mungu ibariki Jamboforum

Amen!
Hio dua na ipokewe!
 
Najua mnaongoza, hongereni, ila mtakamatika tu hivi punde.

Hii season itakua tamu sana, mimi binafsi pia nisingependa kuona timu moja ikipanua gap kubwa kwa juu, I want the excitement till the final day.Lets just enjoy it.
 
Hii season itakua tamu sana, mimi binafsi pia nisingependa kuona timu moja ikipanua gap kubwa kwa juu, I want the excitement till the final day.Lets just enjoy it.

Of course unachokiongelea kina pointi sana, kwamba kunapokuwa na pengo dogo la pointi mshike mshike unakuwa mkali sana. Na ndio hapo vurugu katika mechi zinakuwa haziishi, kufanyiana faulo kunakuwa hakuishi kwani kila mtu anataka kuziba engo hilo dogo, nk. Kumbuka mechi za Arsenal Vs Man U mwaka 2005, mlipomaliza msimu bila kupoteza mechi! Ndio hapo ndugu zenu kina Vieira, Ljungberg, Bergkamp na Wiltord walipoanza kuwategua akina Sylvester viuno. Mechi zinakuwa kaziishi bila ngumi.
Tutarajie majeruhi wa kumwaga sana msimu huu!
 
Leo vp wajameni,
Akiteleza aseno tunarudi kileleni!

Sijui mwanangu, mechi za leo si haba, ni ngumu. Aston Villa waliwakaba koo Arsenal walipokutana mechi iliyopita katika mzunguko wa kwanza, sijui leo itakuwaje. Adui mwombee njaa, ningependa na leo wakabwe koo ili tuwe juu!
 
na kweli basi leo adue wetu tumewaombea njaa naona wakapata janga kabsaaa...wamelala kwao tena kwa kamoooja tuu walishindwa kukachomoa nasie tukawatundika fulhamuuu sijui hamu ya nini bao tatu tuu

anaza cleansheet

msimu wa mwaka huu kweli ni moto wa kuoea mbaliii
 
duh kuja kuhamaki kumbe hawa mdebwedo walikapata kamooja ka ngama na kufanikiwa kuchomoa...maana kaliwangangania hako leo...wangelala naloo..bahati yao lakini still now ni 1pt diff from 5pts zilivyokua..msimu wa mwaka huu raha sana
 
duh kuja kuhamaki kumbe hawa mdebwedo walikapata kamooja ka ngama na kufanikiwa kuchomoa...maana kaliwangangania hako leo...wangelala naloo..bahati yao lakini still now ni 1pt diff from 5pts zilivyokua..msimu wa mwaka huu raha sana

Vijana washika bunduki wamechomoa dakika ya 93, imenikera kinoma!
Lakini hata hivyo nawapa 5 kwa kutuongozea ligi!
Kimbembe kinaendelea.
Wakanyage twende!
 
Jana tulishinda vizuri sana, Yule kijana wa KiKorea alinifurahisha sana baada ya kuweka bichwa wavuni, yaani ukitaka kuwabagua vijana hawa ili umsifu mmoja kuliko mwengine, hilo naona kama haliwezekani kwa Man U. Vijana wote wanasakata kabumbu maridadi sana, Owen alinifurahisha sana baada ya kuniinua katika Kochi nililokaa na kuwacha kahawa yangu ipowe kutokana na furaha ya kusherehekea bao hilo, bao lilikuwa maridadi sana, Yaani hawa Man U, wananistaajabisha kwa utaalamu wao. Yaani Ferguson akiamua kumuweka mtu Bench, wale wanaocheza huwa wazuri zaidi, jamaa hii ni hatari kwa Arsenal na Chelsea.Na yule reserve wetu mstaarabu, Mr Fluke dude O'shea huwa ananifurahisha sana anapoingia uwanjani, huwa mara nyingi zaidi huja na matunda maridadi sana.

Real Madrid wanataka kutufujia timu yetu kwa kumchukuwa Ronaldo, I was very dissapointed with that speculation. Wametangaza dau kubwa la mshahara Euro millioni kumi 10 kwa mwaka, hii itamfanya mchezaji wetu aanze kubabaika na dau hilo.
 
Man U kombe la Klabu bingwa jeupeeee!
Olympique Lyonnais tumewatoa jana, tuangalie mbele. Asante Arsenal kwa kuwatoa Milan
 
167 Reactions
Reply
Back
Top Bottom