Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Duh mkuu umeidharau sana timu yetu

Maajabu means possibility ya ushindi ni labda 10℅ kitu ambacho si kweli

May be 55% kwa 45%

Sent using Jamii Forums mobile app
Siidharau mkuu timu tunayokutana nayo toka 2013 hawakos top 4 wamekaa muda mrefu wanajuana wanakocha mzur sisi kocha wetu itakuwa mech ya 6 bado anatafuta muunganiko wa timu ili falsafa zake zuwaaingie ndo mana naona kama spurs ana nafasi kubwa ya kufanya vizur.
 
Kuwa na imani,spurs kwetu huwa anakuwa mnyonge sana,hata kipindi cha Jose tuliwahi kumpiga mechi moja pamoja na ubovu wetu ule. Omba Herrera awe fomu ampoteze eriksen
Unaona sasa tunategemea muujiza ni kuombea tu ndo mana nasema tunapaswa kujiandaa kisaikolojia bado hatuwez kujipambanua kama zile timu top 3 hii ni kutoka na ujio wa kocha wetu ambae anatafuta chemistry ya timu kwanza tukishinda poa hata tukifungwa ni mwanzo wa kujifunza na kutafuta vipaji na timu ya ushindani.
 
Mie nadhani tuwaombee njaa Chelsea na arsenal ili tuingie top 4. Liverpool na man city ishakuwa historia kwa msimu huu kwetu sisi.
maneno yako yapo juu ya mstari nyoofu muheshimiwa, ndio maana kiupande wangu msimu huu sipotezi muda wangu kuzifuatilia liverpool na manchester city pindi wanapokuwa uwanjani kwa sababu matokeo yeyote wanayoyapata athari yake kiupande wetu inakuwa ni hafifu ukilinganisha na klabu nyengine kama chelsea, tottenham hotspurs na arsenal.
muda huu ndio naangalia highlight ya mechi ya jana kati ya manchester city na liverpool, namuona mjomba dejan lovren katika ubora wake.

mechi yetu dhidi ya tottenham hotspurs ndio itazidi kutoa muelekeo halisi wa top 4 msimu huu hususani kiupande wetu sisi kwa sababu kama tutafanikiwa kuwafunga tottenham basi tutazidiwa kwa alama 7 dhidi yao.
kinachonipa imani kuelekea mechi ya spurs wiki ijayo ni kwamba kwa mara ya kwanza baada ya miaka 3 tutaingia uwanjani dhidi ya timu kubwa huku mawazo yetu makubwa ni (kushambulia) na si (kujilinda ovyo).

inatupasa tuweke imani zetu kwa wachezaji na benchi la ufundi, hata mechi ya mwanzo tulishindwa kuimaliza wenyewe mapema kipindi cha kwanza.
 
uzi wa liverpool japokuwa siipendi pia unafanya vizuri sana.

Hahaha, eti japokuwa huipendi.

Eee ndugu yaani sisi pekee ndio tutapata tabu sana,sababu vurugu zao zote wanaiangalia United na si timu nyingine

Na ikitokea msimu huu tukachukua, itakuwa 19 vs 20, itabaki mara moja tuwe level tena, na dalili zilivyo usishangae tukaja kuwapita ndani ya miaka 10.

Tunahitaji kuondoa gundu mara moja tu.
 
Wakuu nisaidieni kitu hapa.

Baada ya Ferguson kuacha kazi ya ukocha kuna role yoyote alipewa kwenye timu?

Naelewa ana influence as a Legend, nachotaka kujua ni kama ana any official role.

Hii imekuja baada ya ubishi kuibuka kijiweni kwamba eti Ferguson ndiye aliyeshauri coaching team ya sasa (the whole bench), na aliyekuwa anaongoza mjadala anasema Fergie ni member wa board. Mimi nimejaribu kuangalia simwoni kwenye board.

Kuna mahali nimeona alikuwa ni Non executive director around 2013 mpaka Van Gaal anatimuliwa, so kama mtasaidia updates tafadhali.

cc: Mc cane, Damushin, Darmian, lukesam, radika, 4G LTE, Daud1990 na wengine wote.
Sir Alex Ferguson anajilia zake pensheni yake isiyokuwa na kikokotoo mkuu.






Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom