Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Jana nilikuwa nacheki mechi na jamaa yangu mmoja hivi,akawa analalamika sana kuwa timu yetu bado inaruhusu wapinzani kushambulia,mimi nikamuuliza ni timu gani inacheza mechi zote bila kupata sekeseke kutoka kwa wapinzani??..analilia tu clean sheet..yaani akawa ananiboa kinoma..Man city,chelsea,spurs wote hawa gemu nyingi tu hawana clean sheet recently.


Mimi nachoweza kusema ni kuwa mabeki tulionao itafika time tutapata pair nzuri na watakuwa na hizo clean sheet,but for the mean time sisi tuendelee kufunga magoli kama mvua..

Replacement zinaweza kufanyika baadae kwenye baadhi ya maeneo lakini kwa sasa kikosi hiki bado tunaweza kudeliver vizuri tu..


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Sijui ubora wa defence yetu huwa tunaulinganisha na wa timu gani. City wanapunguza mashambulizi langoni mwao kwa kiungo chake kukaa na mpira muda mrefu,lakini nafasi chache wanazopata wapinzani ederson anakufa tu.
Kiungo kikikubali,automatically hata ulinzi utaboreka tu.
 
True that..hata uwe na beki wazuri duniani wote kwenye defence line,kama kiungo kinatetereka na lazima upigwe goli nyingi tu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi habari za man u kuwa na weak defense hazina mashiko wakati wa JM Man u ilikuwa ina defend na wachezaji 11, wote wanabanana na DEGEA kwenye 18 na tulikuwa tunafungwa.

leo tumepunguza idadi ya madefender wetu kwenye 18 yetu tunashinda mechi watu wanalalamika,
our philosophy ni attach attach attach attach attach no time for defending.
 
Jamani Nawasalimia.

GGMU...




Sent using Jamii Forums mobile app

Yani Mkuu navuta picha kipindi kile wewe peke yako unaendesha Kampeni ya Kufukuzwa Mourinho halafu watu wanakushambulia na kukuita Hujui mpira, Unaandika pumba, Mara kama humtaki Mourinho hama timu!!


Leo hii kila Mshabiki Wa Man United hapa anajifanya nayeye alishiriki katika kuendesha Kampeni za kumfukuza Mourinho kuliko Hata wewe 😀😀

Tena kuna wengine wanajifanya sasahivi kusema eti Mourinho anafaa kushtakiwa wakati walikuwa wakimtetea na kukushambulia wewe


Kuna mjinga mmoja anaingia kimyakimya humu anaona haya ata kupongeza ushindi Wa OGS kutokana na misifa aliyokuwa akimpa Mourinho na Kukushambulia wewe. 😀
Inaonesha anasubiri Man United iteleze game moja tu aibuke hapa! 😀😀

Hongera Mkuu Anti-Mourinho Campaign Manager wa JF.
 
Hatimaye kikokotoo kipya kilichokataliwa nchini Tanzania chaanza kutumika nchini Uingereza chini ya ukokotozi makini wa Manchester United.
 
Tuna tatizo Katika Beki yetu, hili lipo wazi, Hatuna right Beki Nzuri, Valencia na Young umri umeshawatupa, Dalot bado.

Tunahitaji fullback mmoja wa ziada tukiendelea kutafuta combination Nzuri ya waliopo, kuna improvement Nzuri kwa Lendlof.

Naamini bench letu la Ufundi litafanyia Kazi mapungufu yaliyoonekana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…