Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

IMG_20181223_083759.jpg
 
Kuna issue ya Technical Skills na Management Skills, kuwa manager mzuri ni zaidi ya kuwa na technical skills. Mara nyingi sana makocha huwa wanazidiwa mbinu na wasaidizi wao, ila wasaidizi wanachokosa ni hiyo Management Skills, kwa hiyo wanaendelea kuwa wasaidizi.

Angalia hata maofisini, wale watu ambao ni mabosi siyo kwamba ni wazuri sana utendaji isipokuwa ni ujanja wa kiuongozi. Kazi wanafanya wengine yeye anaiwasilisha kama ndiye aliyeifanya.

Hapo nimecheka sana! Kwani hata Mimi Kazini kwangu naandaa ripoti/taarifa ya Activity, halafu Mwisho Naandika jina la Mkurugenzi Mtendaji na Anaisaini yeye na kugonga Muhuri wake, Baadae anaipeleka Kwa RAS au TAMISEMI kuwa yeye ndiye aliyeiandaa. 😀😀
 
Raha juu ya raha,huwezi kuamini team ile ile wachezaji wale wale mpira tofauti kabisa.
Jose anastahili kupelekwa ICC😂😂😂
Nilikuwa nawashangaa sana watu wanaolalama José hajapewa anachotaka,ooh mara wachezaji wetu ni wakawaida sana,wakati nikiangalia naona vipaji tupu. Ukilinganisha timu iliyopo sasa na ile aliyotwaa nayo ubingwa babu kwa mara ya mwisho unaona hii ndio ina mafundi.
 
Kweli mkuu jana walijiachia sana nawaza kama bodi ingekubali martial auzwe kwenda chelsea kisha tumchukue willian walahi ilikuwa biashara kichaa kwa upande wetu maana willian 30+ halafu martial under 24 chelsea wangefaidika sana kwa mpira aliocheza jana alikuwa vizur sana tukiimarisha na upande wa mabek mwanga unaonekana.
Willian mwenyewe kwa sasa anarukuruka tu huko chelsea..Akili za mourinho bana..eti anamtaka Maguire,Perisic ili awafunge westham!!...awfull manager
 
Back
Top Bottom